Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Kama hauna au hauko vizuri kiuchumi utumwa unakunyemelea katika muktadha wowote ule. Ndiposa nakuja na ushauri huu kwa jinsi ya ke kuwa wajitahidi kujiimarisha kiuchumi na kutokuwa tegemezi katika jinsi ya Me ili waondokane na utumwa katika mahusiano na katika Ndoa.
Yapo mawazo mgando kuwa wanawake wenye alimu au uchumi mzuri hawaolewi! Hayo ni mawazo ya kikale yasiyo na nafasi katika jamii ya wanamabadiliko.
Mwanamke nivyema ukajitengenezea Nafasi ya kujimudu mwenyewe kiuchumi katika kipindi Cha maisha yako ili usiwe tegemezi au mzigo kwa jamii na kukwepa kutumikishwa. Na Kufa kwa Uhuru wako.
Vilevile itakupa nafasi kushiriki kikamilifu katika harakati za kuhudumia familia na mwenza wako, kushiriki katika kuinua uchumi wa nchi n.k
Karibu kwa maoni