Wanawake, jipambeni kwa mavazi ya kusitiri mwili

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Katika ulimwengu wa leo, mitindo ya mavazi imegeuka kuwa uwanja wa mashindano ya kuonyesha miili badala ya kuonyesha heshima, adabu, na utu wa mwanamke. Kinachosikitisha ni kwamba hata wanawake wanaodai wanamjua Mungu sasa wamekumbatia mavazi mafupi, suruali za kubana na mavazi yanayoacha wazi tumbo na kifua. Wengine wanapenda "kuvaa kwa staili" lakini hawajui kuwa staili hizo zinapotosha maadili ya jamii, kuharibu heshima yao wenyewe, na kuwashawishi wengine kutenda dhambi.

Athari za mavazi yasiyositiri mwili ni zipi?
1. Ni kupoteza heshima yako binafsi: Mwanamke anayefunika viungo vyake visivyopaswa kuonekana anatambulika kuwa mwenye heshima na wa kuaminika. Lakini anayejianika hadharani hupoteza thamani mbele za watu na anaweza kuchukuliwa kama asiyejitambua.

2. Ni kuwa chanzo cha dhambi kwa wengine: Mavazi ya aibu yanawatia watu majaribuni. Yesu anasema katika Mathayo 5:28
"Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Mwanamke anayefunika vema viungo vyake husaidia wanaume wasijikwae kwa kutazama na kuhesabiwa wazinzi.

3. Ni kujikosesha kibali mbele za Mungu: Mungu anaangalia moyo, lakini pia anataka miili yetu tuitumie kwa utukufu Wake (1 Wakorintho 6:20).

Athari kwa Wanaume:
Wanaume wengi wanakiri kwamba wanapomwona mwanamke aliyevaa nusu uchi au mavazi ya kubana, mawazo yao huanza kupotoka, na tamaa ya mwili huibuka. Katika mazingira ya ibada, kazini au mitaani, mavazi yasiyo ya heshima huwafanya wanaume kuyachafua macho yao na mioyo yao. Jambo hili linawasukuma wengi kutenda dhambi kwa mawazo, au hata kwa matendo.

Tunajifunza nini kutoka kwa wanadamu wa kwanza Adam na Hawa?
Katika Mwanzo 3:7, tunasoma kwamba baada ya kula tunda walilokatazwa, "walitambua kuwa walikuwa uchi; wakashona majani ya mtini wakajifanyia nguo." Lakini Mungu hakukubali mavazi hayo ya kujitungia. Badala yake, “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.” (Mwanzo 3:21). Hii inaonyesha kuwa Mungu anatilia mkazo mavazi ya staha, si ya kujionyesha au kuchochea tamaa.

Je, unayajua haya?
Mavazi ni huduma: Unapovaa kwa staha, unamtumikia Mungu na jamii kwa kueneza ujumbe wa usafi wa moyo.

Watoto hujifunza kutoka kwako: Mama anayevaa kwa staha huwalea watoto wake katika misingi ya heshima.

Usifuate mitindo ya dunia: Warumi 12:2 inatufundisha tusiifuatishe namna ya dunia hii, bali tubadilishwe kwa kufanywa upya nia zetu.

Mwanamke mcha Mungu ni kama taa inayong’aa gizani. Mavazi ya heshima si udhaifu, bali ni ushindi wa kiroho na wa kimaadili. Jipambe kwa staha, kwa adabu, na kwa mavazi yanayompendeza Mungu. Urembo wa kweli hauko kwenye kuonyesha ngozi, bali katika kuonyesha tabia njema na hofu ya Mungu. Barikiwa!!
 
Unajifunza nini katika Andiko hili?
1 Petro 3:3-4

"Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu."
 
Katika ulimwengu wa leo, mitindo ya mavazi imegeuka kuwa uwanja wa mashindano ya kuonyesha miili badala ya kuonyesha heshima, adabu, na utu wa mwanamke. Kinachosikitisha ni kwamba hata wanawake wanaodai wanamjua Mungu sasa wamekumbatia mavazi mafupi, suruali za kubana na mavazi yanayoacha wazi tumbo na kifua. Wengine wanapenda "kuvaa kwa staili" lakini hawajui kuwa staili hizo zinapotosha maadili ya jamii, kuharibu heshima yao wenyewe, na kuwashawishi wengine kutenda dhambi.

Athari za mavazi yasiyositiri mwili ni zipi?
1. Ni kupoteza heshima yako binafsi: Mwanamke anayefunika viungo vyake visivyopaswa kuonekana anatambulika kuwa mwenye heshima na wa kuaminika. Lakini anayejianika hadharani hupoteza thamani mbele za watu na anaweza kuchukuliwa kama asiyejitambua.

2. Ni kuwa chanzo cha dhambi kwa wengine: Mavazi ya aibu yanawatia watu majaribuni. Yesu anasema katika Mathayo 5:28
"Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Mwanamke anayefunika vema viungo vyake husaidia wanaume wasijikwae kwa kutazama na kuhesabiwa wazinzi.

3. Ni kujikosesha kibali mbele za Mungu: Mungu anaangalia moyo, lakini pia anataka miili yetu tuitumie kwa utukufu Wake (1 Wakorintho 6:20).

Athari kwa Wanaume:
Wanaume wengi wanakiri kwamba wanapomwona mwanamke aliyevaa nusu uchi au mavazi ya kubana, mawazo yao huanza kupotoka, na tamaa ya mwili huibuka. Katika mazingira ya ibada, kazini au mitaani, mavazi yasiyo ya heshima huwafanya wanaume kuyachafua macho yao na mioyo yao. Jambo hili linawasukuma wengi kutenda dhambi kwa mawazo, au hata kwa matendo.

Tunajifunza nini kutoka kwa wanadamu wa kwanza Adam na Hawa?
Katika Mwanzo 3:7, tunasoma kwamba baada ya kula tunda walilokatazwa, "walitambua kuwa walikuwa uchi; wakashona majani ya mtini wakajifanyia nguo." Lakini Mungu hakukubali mavazi hayo ya kujitungia. Badala yake, “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.” (Mwanzo 3:21). Hii inaonyesha kuwa Mungu anatilia mkazo mavazi ya staha, si ya kujionyesha au kuchochea tamaa.

Je, unayajua haya?
Mavazi ni huduma: Unapovaa kwa staha, unamtumikia Mungu na jamii kwa kueneza ujumbe wa usafi wa moyo.

Watoto hujifunza kutoka kwako: Mama anayevaa kwa staha huwalea watoto wake katika misingi ya heshima.

Usifuate mitindo ya dunia: Warumi 12:2 inatufundisha tusiifuatishe namna ya dunia hii, bali tubadilishwe kwa kufanywa upya nia zetu.

Mwanamke mcha Mungu ni kama taa inayong’aa gizani. Mavazi ya heshima si udhaifu, bali ni ushindi wa kiroho na wa kimaadili. Jipambe kwa staha, kwa adabu, na kwa mavazi yanayompendeza Mungu. Urembo wa kweli hauko kwenye kuonyesha ngozi, bali katika kuonyesha tabia njema na hofu ya Mungu. Barikiwa!!
MUNGU akubariki sana sana!! akutumie zaidi katika ulimwengu wa sasa uliojaa dhambi kuwafungua wengi waliofungwa na shetani.
 
Back
Top Bottom