antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Swali: Kutongoza ni nini?Nakumbuka niliwahi kuingia kwenye mahusiano na binti mmoja wa ki Arusha ambae tulijuana kupitia social media, yeye alikua Arusha na mimi nilikua Dar es salaam
Huyu binti kwanza alikua ananikera kitu kimoja, anapenda sana video call sasa sijui alikua anataka kugundua nini
Ingawa nilikua sipendi lakini nikaona anyway kwakua ndo tumeanza mahusiano wacha nimlizishe
Hali hiyo haikunisumbua sana mana nikajua kadri tutakavyozoeana nitamueleza ukweli kwamba mimi sio mpenzi sana wa video call
Tulipanga kuonana na nilimuahidi kwamba ningeenda Arusha kuonana nae
Huyu binti alinivunja moyo kitu kimoja, kabla hata sijaenda kuonana nae kwa mara ya kwanza akanipiga mzinga wa 80k akidai kioo cha simu yake kimepasuka hivyo anataka akakibadirishe.
Alivyonambia hivyo tu nikaona hapa hamna mtu, yani hata kuonana physically kwa mara ya kwanza bado hatujaonana lakini nishapewa invoice ya 80k wakati yeye mwenyewe anafanya kazi na ana kipato.
Nilikua na uwezo wa kumpa ile hela lakini niliona mbona mapema sana kashaanza kuleta matatizo yake it means yupo after something.
Huyu binti nilimkatia mawasiliano 100% mana niliona hana tofauti na Golddigger na safari yenyewe nilii cancel
Ni kweli wanawake mnahitaji kuhudumiwa na wawanaume ila jitahidini kuficha shida zenu mwanzoni tu mwa mahusiano mana mtajikuta watu wanapiga kisha wanatembea yani ni kama vile kununua malaya Riverside kisha kila mtu anachukua hamsini zake.
Jibu: Kutongoza ni kumbembeleza mwanamke akubali shida zake ziwe zako!
Hutaki unaacha tu..