Wanawake:Kuna uhusiano gani kati ya matumizi ya mafuta mengi na chakula kuwa kitamu?

Wanawake:Kuna uhusiano gani kati ya matumizi ya mafuta mengi na chakula kuwa kitamu?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaa wana Mapishi.

Mimi ni mmoja wa viumbe ambao hawapendi mafuta na chakuLa kinacho zidi mafuta huwa sili. Lakini nimekuwa nikijiuliza chakula kitamu au kizuri ni kile kilicho ng'arishwa na mafuta mengi? Na chakula hakiwezi kuwa kitamu bila kung'aa?

Kuna sehemu fulani nilikaribishwa na nili ambiwa chakuala tayari kwakeli nilivyo funua hot pot daaa nilikutana na nyama iliyo sheheni mafuta,daaa kama haitoshi wali nao ulikuwa umeshehemi mafuta ya kutosha.

Kwakweli siku hiyo nilikosa raha ya chakula japo ilinibidi nile kidogo maana pengine ingeleta picha hisiyo nzuri kwa wenyeji wangu.

Cha kushangaza zaidi Mpishi wa siku hiyo alisifiwa sana na kuambiwa amepika chakula cha hadhi ya hotel na kitamu sana.
daaa kwekweli niliendelea kujiuliza hivi Chakula kizuri au kitamu lazima kisheheni mafuta?

Na hili kama limekuwa tatizo au tabia ya wapishi wengi majumbani ,Migahawani na kwenye mabaha,matumizi ya mafuta mengi yamekuwa kama fashion na ndio kuPendezesha chakula?

Kuna mtu mwingine alinikaribisha chakula na huyu nilimwambia mapema kabisa huwa sipendelei mafuta na akasema hakuna shida.

Lakini nilipo fika mezani duu nilishangazwa kuambiwa kuwa mafuta haya si mengi na hata nyama nilishindwa kula maana kwakweli mafuta yalikuwa mengi.

Nilicho gundua kuwa ni vigumu kutenganisha matumizi ya mafuta mengi na Mapishi ya wanawake walio wengi.

Mimi nilisha acha kula nyama iliyo ungwa kwa mchuzi maana katika mboga inayo washinda wanawake wengi kuweka mafuta kiasi ni nyama.

Unaweza kukuta mtu ana kula chakula midomo ina ng'aa huku mikono ina churuzika mafuta!

Yani bado najiuliza hivi Mapishi bila mafuta mengi hayawezekani?

Wanajamvi wote mnakaribishwa kuchangia, hilo neno wanawake lisi wabane,nimelitumia hili kuonesha msisitizo maana mara nyingi wanawake ndio wanakuwa wapishi.

Wanaume wenzangu nanyi mna karibishwa maana najua nanyi huwa mnapika na wengine huwa mnawasaidia akanana kupika.

Mimi huwa napika lakini wale wapenzi wa mafuta mengi mimi ni adui yao namba moja.

Karibuni Wana Mapishi.
 
si dhani na ukiangalia hotel kubwa kubwa au hata vipindi vya mapishi utaona unaambiwa weka mafuta kidogo kijiko kimoja au viwili, na mbona chakula kina kuwa kitamu tuu, maana kama mafuta ya sunflower ukiyajaza kwenye chakula unaweza kushindwa kukila chakula hata kama ni kitamu vipi
 
Vyakula vitamu vingi ni vya kuchemsha na ku bake....

Chipsi ya kukaanga na mafuta sio tamu sana kama za ku bake shoga angu King'asti nadhani utanisapoti...

Vyakula vya mafuta huwezi kula ukashiba vizuri vyakinaisha haraka......

Nakusapoti kwa kweli watu wengi wanafkiri upishi mzuri ni kupika kwa kutumia mafuta mengi au kukarangiza......

Wengi humu pia nimepepeleza wanapenda rosti ila ukijaribu chukuchuku siku moja tu kwa rosti utahama wallah.......
 
Last edited by a moderator:

Au extra virgin kwenye salad ni nzuri and very healthy na yasaidia chakula kusagwa kwa ufanisi zaid
 
Hataa maandazi ya kukaanga hayanogi sana kama ya kubake......huwa nusy nakaanga nusu na bake...
 
Attachments

  • 1401906559523.jpg
    1401906559523.jpg
    104.2 KB · Views: 258
  • 1401906576078.jpg
    1401906576078.jpg
    76.3 KB · Views: 256
si dhani na ukiangalia hotel kubwa kubwa au hata vipindi vya mapishi utaona unaambiwa weka mafuta kidogo kijiko kimoja au viwili, na mbona chakula kina kuwa kitamu tuu, maana kama mafuta ya sunflower ukiyajaza kwenye chakula unaweza kushindwa kukila chakula hata kama ni kitamu vipi
Mkuu pamoja nakusema haya yotE ni tofauti na yanayo tendeka kwenye jamii zetu hasa kwenye Vyakula nilivyo vitaja!
Mafuta mengi imekuwa fashion.
 
Hataa maandazi ya kukaanga hayanogi sana kama ya kubake......huwa nusy nakaanga nusu na bake...
Vyakula ulivyo vitaja farkhina mara nyingi mafuta mengi haya tumiki lakini vyakula kama wali,nyama ndizi ndio huwa ni tatizo kabisa na jamii zetu ni mashahidi.

Kwenye hivyo vyakula ni mara chache sana kukuta vimepikwa kwa mafuta kiasi.

Wewe farkhina uhusiano wako na mafuta kwenye mapishi hasa kwa vyakula nilivyo vitaja hukoje?
 
Last edited by a moderator:
Vyakula vitamu vingi ni vya kuchemsha na ku bake....

Chipsi ya kukaabga na mafuta sio tamu sana kama za ku bake shoga angu King'asti nadhani utanisapoti...m.

Vyakula vya mafuta huwezi kula ukashiba vizuri vyakinaisha haraka......

Nakusapoti kwa kweli watu wengi wanafkiri upishi mzuri ni kupika kwa kutumia mafuta mengi au kukarangiza......

Wengi humu pia nimepepeleza wanapenda rosti ila ukijaribu chukuchuku siku moja tu kwa rosti utahama wallah.......
Daaa wengi wanaaamini kwenye
mafuta mengi siui kwanini?
 
Last edited by a moderator:
Vyakula ulivyo vitaja farkhina mara nyingi mafuta mengi haya tumiki lakini vyakula kama wali,nyama ndizi ndio huwa ni tatizo kabisa na jamii zetu ni mashahidi.

Kwenye hivyo vyakula ni mara chache sana kukuta vimepikwa kwa mafuta kiasi.

Wewe farkhina uhusiano wako na mafuta kwenye mapishi hasa kwa vyakula nilivyo vitaja hukoje?

Heee yani mafyta mengi hadi ukiigida wawea jipaka mwili mzima na yakabaki lol.....

Siweki mafuta mengi kwetu watu wanaogopa vitambi na unene siku yakiniponyoka wananisema mpakaaa.....

Ndizi hiyo apo just nlitumia 3 tablespoon ya mafuta...
 
Attachments

  • 1401908488338.jpg
    1401908488338.jpg
    18 KB · Views: 237
Last edited by a moderator:
Heee yani mafyta mengi hadi ukiigida wawea jipaka mwili mzima na yakabaki lol.....

Siweki mafuta mengi kwetu watu wanaogopa vitambi na unene siku yakiniponyoka wananisema mpakaaa.....

Ndizi hiyo apo just nlitumia 3 tablespoon ya mafuta...
Haaaa hizi ndizi......
Ila mafuta yampaka unajipaka ni hatari sasa.
 
Ignorance na uvivu wa kutafuta recepies nzuri zisizotaka mafuta. Weekdsys nakula raw foods weekend nakula cha "
mafuta" home
Mi nafikiri sababu ni mazoea ya kupenda mafuta.
 
Nadhani kinachokushinda kula nyama za kuungaa si kwamba wakati wa kuunga wanatia mafuata mengi,bali watu wengi wanaponunua nyama wakati wa kuiandaa ua hawatoa yale mafutafuta ya kwenye nyama,ni vizuri kutoa yale mafuta halafu ukaichoma kidogo kuondoa yale majimaji mekundu,kisha ukaichemsha na kisha kuiunga!! Hakika hautokinai kula nyama ya mchuzi.
 
Vyakula vitamu vingi ni vya kuchemsha na ku bake....

Chipsi ya kukaanga na mafuta sio tamu sana kama za ku bake shoga angu King'asti nadhani utanisapoti...

Vyakula vya mafuta huwezi kula ukashiba vizuri vyakinaisha haraka......

Nakusapoti kwa kweli watu wengi wanafkiri upishi mzuri ni kupika kwa kutumia mafuta mengi au kukarangiza......

Wengi humu pia nimepepeleza wanapenda rosti ila ukijaribu chukuchuku siku moja tu kwa rosti utahama wallah.......

dada chips za kubake znapikwaje?nataman kujua
 
Last edited by a moderator:
mafuta mengi wakati wa 6 x 6 ....mpishi lazima atakuwa na tatizo
 
Back
Top Bottom