Wanawake:Kuna uhusiano gani kati ya matumizi ya mafuta mengi na chakula kuwa kitamu?

Wanawake:Kuna uhusiano gani kati ya matumizi ya mafuta mengi na chakula kuwa kitamu?

Mafuta mengi hayanogeshi chakula zaidi ya kukifanya kikinaishe wakati wa kula.

Mimi hata nikipika mchuzi wa mafuta nakaanga vya kukaangwa then natoa mafuta yote ndo namalizia kuweka viungo vengine.

Hata supu ya nyama au kuku nikiona mafuta yanaelea juu inanishinda kula kabisa.
 
utakuta mtu anatumia zaidi ya lita tano ya mafuta ya kupikia kwenye familia ya watu watano tuu.
Madhara yake ni makubwa kuliko watu wanavyo fikiri.
  1. matumizi mabaya ya pesa.
  2. Ni rahisi kwa familia kuto kuishi kwa furaha kwa muda mrefu kwani magonjwa kama ya moyo, pressure yatawaandama wanafamilia na mwisho kusababisha vifo.
  3. Cholesterol ambayo ni mbaya sana inayopatikana kwenye mafuta kwani kwa mtu wa kawaida kudhaminisha ubora wa mafuta sio rahisi japo brand nyingi wameandika cholesterol free.
Ukweli elimu inahitajika sana kwa wapishi wa majumbani kuhusiana na mapishi.
Binafsi nikishaona mafuta tuu kwenye chakula nakua mkweli kua situmii mafuta mengi bila kujali aibu kwa wenyeji.
 
Pole sana Ruttashobolwa

Bahati mbaya baadhi ya wanawake wanadhani kuwa mafuta ndio mapishi.

Chakula kinahitaji mafuta kidogo sana kinachotakiwa ni ubunifu wa mpishi hususan kwenye kuweka viungo na mpangilio wa ladha.

Na kwa faida ya wengine kuna baadhi ya sehemu za nyama huwa na mafuta mengi. Hivyo ni vyema kabla ya kuunga ukamwaga mafuta ya nyama na usitumie mafuta kabisa(haswa kwa sie tusopenda michuzi)
 
Last edited by a moderator:
dada chips za kubake znapikwaje?nataman kujua

Kuna namna nyingi za kuzipika.
Mie hukata viazi kama kawaida

Paka bakin tin yako olive oil kidooogo Then nanyunyuzia chumvi kidogo, pilipili manga na swaumu kidunchu kama utapenda (maana ikiungua huwa chungu, sishauri saaana kwenye swaumu) tia kwenye oven.

Hutotamani tena chips za mafuta ukianza kula hizi
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Kuna namna nyingi za kuzipika.
Mie hukata viazi kama kawaida

Paka bakin tin yako olive oil kidooogo Then nanyunyuzia chumvi kidogo, pilipili manga na swaumu kidunchu kama utapenda (maana ikiungua huwa chungu, sishauri saaana kwenye swaumu) tia kwenye oven.

Hutotamani tena chips za mafuta ukianza kula hizi

Asante best, nitajaribisha na mimi ushamba unitoke....lol
 
Back
Top Bottom