Wanawake kuota Ndevu na Vipara: Chanzo, tahadhari na tiba yake

Jamani Mungu ana-balance mambo.Kila siku wenzetu wanapigania gender equality.Haya sasa tuanze na ndevu.
 
Ni side effect za mkorogo.kwa tanzania, Mbeya ni mkoa unaoongoza kwa wanaopaka mkorogo,ukienda Kyela,Tunduma na hata Mbeya Mjini utabaki mdomo waaaazi hinsi kina mama walivyogaribika kwa mkorogo.

Sijajua sababu ni nini hasa inayopelekea kuupenda mkorogo,labda ya kuwa vipodozi vingi vya kujichubua vinatokeo huko kutoka Congo,Malawi na Zambia.

Mkoa unaofuatia kwa mkorogo ni Tanga,sababu kwa mkoa wa Tanga ni kuupenda weupe na uarabu, wakipaka hina ionekane,maana ngozi nyeusi hina haionekani vizuri.

Ila Njombe nako hawajambo,weupe asilia ni kitu adimu, nao kwa mkorogo wanashika chati.
 
Niko hapa Mbeya maeneo ya soweto kwenye moja ya grocery napata konyagi ameingia mama mmoja ana ndevu na mustachi halafu usoni sio mweupe bali ni mwekundu,Lakini nimeuliza nikaambiwa ni mkorogo....!

Konyagi na kiti mito tamu sana mkuu,nasikia hapo bei poa sana hapa mza kg 1=9000
 
mimi napita tu ina maana hata yule msemaji wa polisi naye ni wa MBEYA?
 
Labda baridi...teh teh

Hakuna sehemu ambayo ina baridi kama mafinga, makambako na makete. Mbôna huko hawaoti ndevu kiasi hiki? Naweza kubaliana kiasi na wanaosema mkorogo maana wanawake wa mbeya wengi nyuso zao ni nyekundu ila shingoni kuna ukurutu. Lakini kuna wengine wana rangi asili na videvu vyao vimechafuka,why?
 
Nadhani ni maumbile na pia inategemea ukoo na ukoo, kwa upande wa mama zangu kuna baadhi yao wana ndevu lkn upande wa baba hakuna mwanamke hata mmoja mwenye ndevu
Ndio maana nikauliza, nini
kinasababisha watu wa aina hii kuwa wengi? Na kwa nini mbeya ni wengi
zaidi?
 
Basi sijui
 
Nami nichangie hii mada kwa kutoa mawazo yangu kulingana na hisia zangu maana ni kweli wanawake kuwa na ndevu ni jambo jipya katika jamii.

Bila shaka mnaweza kulinganisha suala hili na vizazi vilivyopita kama vile mabibi zetu wa pande zote mbili. Utaona kwamba kamwe suala hilo hata wao wanaliona ni geni, ninachoweza kuona kuna ukweli kuhusu hilo ni matumizi ya mafuta ya kupaka mwili hususani lotions.

Kama tujuavyo kuna kitu inaitwa diproson mafuta haya yalitumika kwa wingi sana miaka ya 1970's na 1980 hadi pale yalipopigwa marufuku kutumika kutokana na kuwepo kemikali hatari. Matumizi haya yalikuwepo kwa wingi sana sehemu za mipakani hususani Mbeya-Zambia, Mbeya-Malawi.

Ukiona watumiaji wa mafuta haya wa miaka hiyo leo hii wanahudhuria tiba ya maradhi ya ngozi pale Ocean-Road Hospital aidha kwa kuhisi wana saratani au tatizo la ngozi.

Wengi wao sasa ni watu wazima. Hata hivyo hawawezi kuwatahadharisha watoto wao na watu wengine kuwa kuna uwezekano kwamba matatizo yao yanatokana na matumizi ya mafuta hatari kama diproson.

Madhara mojawapo yanayoendana na matumizi ya mafuta ya namna hii ni kuharibu mfumo halisi wa utendaji wa ngozi ya mtu husika, wengi wa wanawake utawaona siyo tu kuwa na ndevu bali kuwa na vinyweleo vingi mwili mzima. Sipendi kuwataja wanawake wenye ndevu lakini hebu piga picha.

Matumizi mabaya ya mafuta yaliyozuiwa husababisha mabadiliko katika hedhi kwa wanawake hili nalo limekuwa likienda sambamba na uotaji ndevu kwa wnawake, sielewi kwanini sijafanya utafiti.

Ili kujiridhisha sisi sote tufanye jambo moja ukimuona mwanamke mwenye ndevu kaa naye kisha muulize historia yake ya maisha, anasa zake, kula kwake matumizi ya vipodozi na mengine.

Bila kusahau matatizo yake kiafya ni yepi, uzito wake wa mwili maana ukiwaona wanawake wengi wenye ndevu wengi wao ni wanene.
 
Kiujumla siku hizi wanawake wengi wana ndevu...mimi imenishangaza sana...
 
Dawa mpya kabisa ya tatizo sugu linalowasumbua wanawake kwa sasa ya kuondoa ndevu dozi kamili kwa mwenye tatizo hilo inachukua Sh 150,000 tuu ni PM ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…