Wanawake kuota ndevu, tatizo hasa ni nini??

Tayukwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2014
Posts
2,178
Reaction score
4,410
Salaam wana JF
Ndugu zangu naomba tusaidiane ktk hili la hawa wenzetu (wanawake) katika kukithiri kwa uotaji wa ndevu.

Miaka ya tisiini hivi nilikuwa na shangazi yangu ambaye yeye alikuwa na ndevu kama tano hivi kidevuni kwake, hali hiyo ilimfanya aishi kwa hofu hasa kipindi anaposafiri kwani alikuwa anahofia kunyolewa ikiwa atalala ndani ya gari kwa zile imani kuwa mwanamke akiwa na ndevu basi zile ndevu zake ukizipata utakuwa tajiri (binafsi naona ni imaan potofu). Sasa tatizo liko hapa, kipindi kile wanawake wenye ndevu walikuwa wachache mno ukilinganisha na miaka hii.

Kisayansi mwanamke akipata baadhi ya homoni za kiume basi huwa na baadhi ya sifa au vitu ambavyo mwanaume anavyo mfano hizo ndevu. Sasa kipindi hiki hizi homoni za kiume zimekuwa nyingi sana kwa wanawake au tatizo ni nini hapa?.
Je, kuna baadhi ya vyakula huchangia hali hii??

Kuna baadhi ya watu nimewasikia wanasema kemikali zilizomo kwenye baadhi ya lotion na cream zao huchangia vipi kuna ukweli wowote katika hili?

Ni umri gani hasa hushambuliwa na janga hili?
Je, nikweli kuwa tatizo hili ni la kurithi?
Je kuna baadhi ya wanawake hufurahia hali hii?

Wanaume mlioowa wanawake ambao wana ndevu na Garden love huwa mna changamoto gani na mna enjoy vipi kwa wake zenu wenye hali hizo?

Jana nilikutana na mdada mmoja akiwa na umri kati ya miaka 19-22 lakini tayari ameshaanza kushambuliwa na hali hii ya kuwa na ndevu, ndipo liliponijia wazo hili la kutaka kupata ufafanuzi wa kina kwa wenye uelewa katika hili.Mfano mwingine ni yule kamanda wa polisi nadhani wa Ilala au Temeke lakini sina hakika sana lakini nae ana tatizo hili.

Tuwashauri nini wafanye ili kukabiriana nalo, na wale ambao hawana kipi au nini wafanye ili kuepuka. Na kinyume chake kwa wale wanawake wote wanaohitaji kuwa na ndevu nini wafanye ili wazipate maana akili zao..........
 
Kwa kweli hili ni janga
 
Binafsi nina ndevu ila sipendi, kwetu tuna asili ya nywele nyingi! Vinyweleo vingi mpaka watu huwa wanatushangaa, nataman nijue dawa ya ndevu tu maana zinaninyima raha hapa nilinyoa juzi leo zishasimama tena
 
Reactions: Luv

usinyoe kabisa ziache
 
Binafsi nina ndevu ila sipendi, kwetu tuna asili ya nywele nyingi! Vinyweleo vingi mpaka watu huwa wanatushangaa, nataman nijue dawa ya ndevu tu maana zinaninyima raha hapa nilinyoa juzi leo zishasimama tena
Photo please.
 
Tatizo Hilo pia ninalo na dada yangu pia lakini mama yetu Jana sasa sijui kama ni kurithi kutakuwa ni kwa baba ama mama maana nimejaribu kufuatilia sijaona meingine kwenye ukoo wetu
 
Tatizo Hilo pia ninalo na dada yangu pia lakini mama yetu Jana sasa sijui kama ni kurithi kutakuwa ni kwa baba ama mama maana nimejaribu kufuatilia sijaona meingine kwenye ukoo wetu
Vipi kuna ukweli wowote kuhusu vitu tajwa hapo juu kwa upande wako
 
Tatizo Hilo pia ninalo na dada yangu pia lakini mama yetu Jana sasa sijui kama ni kurithi kutakuwa ni kwa baba ama mama maana nimejaribu kufuatilia sijaona meingine kwenye ukoo wetu
Vipi kuhusu vipodozi vyako?
 
matumizi ya madawa ya uzazi yanachangia sana. Zikiota zing'oe tu hazioti tena.
Wewe ukiwa kama mwanaume vipi umewahi kung'oa ndevu zako ili kuhakikisha unachokisema?
 
Usinyoe win, utazifanya ziote zaidi sasa
Itambidi azinyoe ili akae vizuri sasa bila kunyoa wewe unaona inakuwa sawa hiyo? pata picha mwanaume ambae hajanyoa ndevu kwa miezi3, vp kwa mtu kama Winlicious
 
Vipi kuhusu vipodozi vyako?
Natumia Vaseline na usoni huwapipaki mafuta yoyote kwa sababu uso wangu unatafuta sana. Huwa napaka poda tu. Na kwa upande wa uzidi wa mpango nikitulia loop (kitanzi) wakati tayari ndevu ninazo.
 
Natumia Vaseline na usoni huwapipaki mafuta yoyote kwa sababu uso wangu unatafuta sana. Huwa napaka poda tu. Na kwa upande wa uzidi wa mpango nikitulia loop (kitanzi) wakati tayari ndevu ninazo.
Uuuwi jamani vipanguso hivi. Nilimaanisaha usoni sipakagi mafuta kwani uso una mafuta sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…