wanawake ndio walivyo mwenyewe nimeshudia ambao nafanya nao kazi salary sawa tukitoka tax nalipa mimi bia nalipa mimi nyama nalipa mimi juzi nikawapa live mkitaka mtoke na mimi mnachangia ngapi? au tuchange sawa kwa sawa, ...... hata aibu hawana
alikua anafanyakazi wakati mm nasoma chuo,lakin mara ninunulie chupi,mara apple mara vitu vidogo vidogo...jibu lilikua eti wanawake wanaona unapotoa kitu kwao ni kama unamthamin na wanapenda.
Anyway sijui kama ni kweli au ulikua utapeli tu kama utapeli mwingine,tusubiri kina dada watatujuza vizuri
wanawake ndio walivyo mwenyewe nimeshudia ambao nafanya nao kazi salary sawa tukitoka tax nalipa mimi bia nalipa mimi nyama nalipa mimi juzi nikawapa live mkitaka mtoke na mimi mnachangia ngapi? au tuchange sawa kwa sawa, ...... hata aibu hawana
Si wanawake wote wako hivo. wanawake wengi tu wanasaidia wanaume zao
Na kama yeye mwenyewe kakuzoesha hivyo utabadilikaje? Embu mie nifaidi zangu maana na nyie mkiona mwanamke anaprovide mnatafuta pengine pa kwenda kuzipunguza. nitasaidia pale nitakapoona nahitajika kwa sasa acha nifanye mambo madogomadogo ya home tu na kujiremba na kuvaa na kusave just incase
nafikiri malezi yetu yamechangia kwa kiwango kikubwa kwamba mwanaume ndie mtoaji/mlezi lakini sikubaliani na hii hoja wote sio watoaji wengine hata kama una kipato bado anaamini mchango wake una umuhimu.
rafiki wangu kizungu namtoa out ananitoa out,namnunulia zawadi ananinunulia zawadi,jinsi tulivyoonza mapenzi yetu,hadi leo sijashika pesa yake na hajashika pesa yangu,,,,,tunaishi kwa amani na upendo.
No matter how much I earn, to me the MAN is provider, so please don't try to change the nature. Unapata respect pale unapospend kwa wife wako au family hata kama kipato ni kidogo.
Ukiwa utakuwa wewe ni mwanaume na utakuwa ni mpokeaji subiri kuitwa mwanaume SURUALI.
nadhani watu wanaanza kusahau asili yao, pengine labda si wote wafuasi wa dini kama yangu.
Kwa kifupi ninachoelewa mimi, mwanaume ni kichwa cha nyumba, atakula kwa jasho lake, ndiye anayetoa posa
Ni wajibu wake kumhudumia mke wake/familia kwa waliooa. Kama mama ana kipato kikubwa, akiamua kuchangia, ni kwa mapenzi yake au makubaliano yao. Vinginevyo msishangae majina kama hayo kwenye red.
Hatuishi kwenye zama za kale..sasa hivi maisha ni kusaidiana!
Siongeli zama, naongelea maagizo ya Mungu. Mwanamke atazaa kwa uchungu, mwanaume atakula kwa jasho. Kumbuka agizo la Mungu pale bustani ya Eden. Sasa kama wewe unapingana naye, ni juu yako.
Nyie ndo wale wenye ideology za 'kazi ya mwanamke ni kuzaa tu' hana sauti wala uwezo wa kufanya zaidi!Biblia pia inatuambia tuwe tunalipiza jicho kwa jicho...sidhani kama ndivyo tunavyoishi!
Kama mwanamke angekuwa ni kuzaa tu, familia nyingi zisingesimama. Zaidi ya hilo wanatafuta kama wanaume, wazijua sababu zilizowafanya nao watafute kwa jasho? Ndo mchango wake mkubwa! Asilimia kubwa ya wanawake wanaplay part ya mwanaume kwa sasa, mwanauma anafanya nini?
Nafurahi kwamba umeshindwa kujibu swali langu na umejigeuka mwenyewe!Kama wanawake wasiposaidiana na wanaume familia nyingi hazitaendelea!
Tayari umesema mwanamke ni msaidizi...sasa kumsaidia mwanaume kunageuka vipi kosa?!?Kuolewa au kutokuolewa kwangu is irrelevant here!Sidhani kama unachokitetea unakijua Lizzy, samahani kwa kusema hivyo. Mwanaume ni wajibu wake kutimiza majukumu yake, mwanamke ni msaidizi tu, na siyo wajibu wake. Usawa wa kusaidia kuzungusha raundi za bia nehiii... kabisa, kuna vitu muhimu vya kufanya katika familia. Labda nikuulize mwenzangu, umeshaolewa?
Tayari umesema mwanamke ni msaidizi...sasa kumsaidia mwanaume kunageuka vipi kosa?!?Kuolewa au kutokuolewa kwangu is irrelevant here!
Usikasirike dia, tunaeleweshana. Inapofika wakati, inabidi tukubaliane kutokukubaliana.