- Source #1
- View Source #1
Kumekuwapo na nakala ya gazeti inayosambaa mtandaobi ikiwa na madai hayo, likiwa na utambulisho wa Botswana Daily.
- Tunachokijua
- Uwaraza ni hali inayotokana na mtu kupoteza nywele za kichwani kwa kiwango kikubwa huku sababu kubwa ikiwa ni kuwa na umri mkubwa. Hali hii inaweza kumpata mtu yeyote lakini mara nyingi imekuwa ikiwatokea wanaume.
Madai
Oktoba, 2026 imeibuka nakala ya gazeti ikiwa na utambulisho wa Botswana Daily ikiwa na ujumbe "Having an affair with bald Men reduces your lifespan". Ikiwa na maana kuwa Wanawake kuwa na uhusiano na wanaume wenye uwaraza kunawapunguzia muda wa kuishi?
Uhalisai wa mdai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kisayansi wa madai hayo. Aidha hakuna uthibitisho kuwa utafiti huo umechapishwa na mamlaka ama chuo huko nchini Botswana.
Gazeti hilo linaonekana kuwa ilikuwa ni nakala ya Machi 10, 2026 lakini uhalisia ni kuwa gazeti hilo ni la kubuni na halina uhalisia wowote. Gazeti hilo lina dosari kadhaa ikiwemo tarehe kusoma Jumatatu Machi 10, 2026 na uhalisia ni kuwa siku hiyo ilikuwa ni Jumanne.
Sambamba na hayo imebainika kuwa gazeti halisi la Botswana Daily lina muonekano tofauti na lilikuwa na ujumbe tofauti kwa siku hiyo tofauti na unaonekana kwenye gazeti la kubuni. Bofya hapa kuona gazeti website ya gazeti halisi.