Wanawake kwa nini mnatudanganya hamjaolewa

Wanawake kwa nini mnatudanganya hamjaolewa

Gamaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2008
Posts
3,915
Reaction score
5,038
Leo siku yangu imeharibika kabisa, kuna huyu mdada niko naye mwaka wa pili sasa kwenye mahusiano kumbe ni mke wa mtu bhana. na siku zote ananiambia hana mume mtoto wake aliye naye baba yake alifariki zamani.

Duuh kumbe mke wa mtu jamaa yake kanipigia simu na mikwala kibao tena ni mtu wa Tanga ananiambia ameniangalia kwa babu yake amekuta mi mwenyewe mweupe kama karatasi, haichukui hata masaa matatu kumaliza kazi na anasema nitampa faida kwa sababu ataenda kuniuza kama msukule huko kwao Tanga.

Nimeogopa kweli imebidi nimuombe msamaha tu. Jamani akina dada kama una mtu tafadhali muwe mnasema haya mambo ya kuwa misukule tena sio poa.
 
Pole, lakini ndiyo kick yenyewe !!

Akikuambia kaolewa utamshusha thamani [emoji38][emoji38]
 
He,he,heh...
Anakutishia tu mkuu, we endelea kujilia utamu.
 
Ngoja nipeleleze, maana nami nimeambiwa bbaba Mtoto kafariki, dada yake aliniambia mume wa huyo mdogo wake...aliolewa na mbibi mmoja ulaya na huwa hatoi matumizi. Kwa maelezo yako nami nakuunga mkono kkujitafutia solution yangu. Single mother wamejaa kila Kona, yaani duh!
 
acha woga wewe unapigwa mikwara kizembe zembe unakubal unajuaje kama sio mchepuko mwenzio
 
Khaa na wewe unakuwa na mahusian miaka 2 yote hiyo unataka kutengeneza rocket inayoenda nje ya anga
 
Mwambie uko na mkewe kwa ajili ya tiba za jadi toka sumbawanga na tayari mmeshafunga ndoa baharini.
Mpaka sasa mna watoto 6 wote wako baharin.
 
Labda anatumia mbinu ya kujifanya 'mume' ukimbie
aingie....muite muonane uso kwa uso na huyo mwanamke
 
Achana nae chukua goma jingne

Mke wa mtu hatari sn
 
Huenda ikawa kaolewa kweli au pia inaweza kuwa kapata mwingine ndio mana katafuta njia ya kukutisha ili uachane naye. Hivyo akili kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom