Wanawake, kwanini huwa mnapambana kumtawala mwanaume kisha kumtenganisha na ndugu zake na rafiki zake?

Wanawake, kwanini huwa mnapambana kumtawala mwanaume kisha kumtenganisha na ndugu zake na rafiki zake?

EL ELYON

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
1,565
Reaction score
1,918
Nipo mkoa Fulani kanda ya ziwa kikazi nilihamishiwa huku kwa bahati nzuri huku nilimkuta ndugu yangu mmoja tunaelewana Sana maana tumekua wote enzi hizo.

Sa kwa vile mi bado mgeni kidogo na ni wale introvert najikuta nipo bored Sana na huu mji mida ya jioni huwa napenda kumcheck ndugu yangu na kutoka naye ingawa si siku zote lakini kuna tabia niliigundua kwa mke wake ni kama hapendi kabisa kuniona pale kwake sijajua ni kwanini ukizingatia sili wala kunywa pale kwake yaani kwa kiifupi sina njaa.

Wakati mwingine namsalimia haitikii au nisipomsalimia ndo imetoka au akinikuta nipo na mumewe hasalimii. Hilo halinisumbui hata kidogo maana mi nishaona mengi sana na nimepitia mengi kwahiyo Yule mwanamke namuona hajai hata kwenye kiganja na matukio yake na hawezi nizuia wala kunipangia kwenda kumuona ndugu yangu.

Cha ajabu wakigombana na mumewe yeye ndo huwa wa Kwanza kunitafuta nikasuluhishe hata saa sita za usiku naenda.
Kilichonifanya nilete haya humu juzi nilipita pale kwake kwani nilikuwa nimeongea na ndugu yangu tapita jioni anisindikize mahali kweli nilipita nikamkuta mkewe nje nikampa salami hakuitikia kisha nikamuuliza huyu jamaa yupo. Akajibu amelala kisha akaendelea na shughuri zake alikuwa anafua mi nikabaki dilemma nikisubiri labda ataenda kumuita lakini hakufanya hivyo.

Hivi wakuu wanawake huwa mna matatizo gani na ndugu upande wa mume? Hivi mnategemea unaweza kumuachanisha mumeo na ndugu zake kweli unaweza ukafanikiwa lakini muda ni hakimu mzuri Sana.

NB: unaweza ukawa na ndugu yako au ndugu zako tena wa damu kabisa mmekuwa pamoja bila tatizo wala kutengana lakini nawaambia atakayekuja kuwatenganisha hata msisalimiane kabisa na mkawa maadui wakubwa ni mke wa mmoja wenu yaani mwanamke. Kama mi muongo naomba ambao mmewahi gundua Hilo mseme hapa.

Fatilieni tukio la wanamuziki P square nini kiliwamaliza jibu ni mwanamke. Kulikuwa na jamaa zangu Fulani walikuwa jirani zetu mtu na Kaka yake mdogo mtu alikuja kwa Kaka mtu kutafuta maisha alipoyapata kidogo akapanga chumba hapohapo alipokuwa anaishi Kaka yake sasa shida ilijitokeza mdogo mtu akapata mwanamke akaoa na Kaka mtu naye akaoa Moto uliwaka aisee kwani mke wa mdogo mtu hakumpenda Kaka wa mume na mkewe ilikuwa vita bahati mbaya mdogo mtu naye kwa mkewe hapindui navyozungumza hapa hawawasiliani wala kusalimiana chanzo MWANAMKE.

Hivi nyie baadhi ya wanawake huwa mna shida gani aisee na ndugu wa mume kwanini huwa mnapambana kumtawala mwanaume kisha kumtenganisha na ndugu zake na rafiki zake wakati hata hujui wametoka wapi? 🤔🤔🤔🤔 KARIBUNI MANA 👇
 
Hawa ndugu bhana ni mabonge ya ERASE kwenye ndoa. wakishafanikisha ajabu ata ndugu yao hawamtaki.

Kifupi hawa wanatumikaga kuimarisha imani yako tuwapigieni makofi tafadhali 👏
 
Hilo halinisumbui hata kidogo maana mi nishaona mengi sana na nimepitia mengi kwahiyo Yule mwanamke namuona hajai hata kwenye kiganja na matukio yake na hawezi nizuia wala kunipangia kwenda kumuona ndugu yangu.

hapo hiyo kauri nimependa sana
na ndio nilochokuwa nafanya kwa mjomba angu
yaan kwa huyo mjomba angu mke wake alikuwa na roho mbaya na hakuwa ananipenda tu mpk leo sijui kwanini hatuivi yaan hatupatani kabisa
halafu mm na huyo uncle tunaelewana sana tangu nipo mdogo yaan ni zaidi ya mtu na mjomba wake ni marafiki
amenizidi kma miaka 15 hivi so tulikuwa na bondi balaa
yaan huyo mkewe pamoja babu na bibi wakawa waananiambia huko utakiwi utavunja NDOA za watu bure usiende
lkn wapi moyoni nikawa nasema hvyohvyo yule mwanamke hawezi mie kunizuia nisiende kwa ndugu yangu mpuuzi tu ninakwenda na tunatia story balaa sasa aliumia zaidi baada mtoto wake wa kwanza kunizoea mno kuliko hata babaake yaan nikienda kwao nikiondoka kilio au wakija home hataki kuondoka atataka abaki na mimi
basi huyo shangazi yangu mke wa mjomba full kununa

hii thread yko imenikumbusha mbali miaka mingi sana miaka 90 huko
 
Yule ni dogo tu halafu Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo wala si dharimu hata Ajute
Kusema tuishi kwa akili na wanawake lazima mtu ujiulize why mwanamke

Takachokifanya ni kulinda ndoa yake tu mi nisiwe chanzo cha kuachika basi ila mengine yote atajua hajui kwenye hiki kichwa. Aliwahi mshikia kisu ndugu yangu kisa eti aliona sms ya mchepuko kwenye simu ya ndugu yangu mbaya zaidi huyo ndugu yangu ni askali si mnajua wengi wao walivyo malaya
 
Sa kwa vile mi bado mgeni kidogo na ni wale introvert najikuta nipo bored Sana na huu mji mida ya jioni huwa napenda kumcheck ndugu yangu na kutoka naye

Kilichonifanya nilete haya humu juzi nilipita pale kwake kwani nilikuwa nimeongea na ndugu yangu tapita jioni anisindikize mahali kweli nilipita nikamkuta mkewe nje nikampa salami hakuitikia kisha nikamuuliza huyu jamaa yupo.

Naomba ni quote hizi aya mbili.
Huyu mwanamke yupo sahihi. Ameshazoea kuishi maisha fulani na mume wake ila tangu uende umembadilisha mume wake, unamgeuza kama chawa wako kila mahali mfuatane[emoji57].

Kwanza wewe umeoa?
 
Hii kitu miaka ya nyuma nakumbuka, shangazi yetu yupo hivyo hivyo,hataki ndugu upande wa mume kabisa kwake yy ni ndugu zake tu. Mjomba kasomesha mashemeji zake na watoto zao, wengine kawatafutia kazi, wengine wakiharibu kazini mjomba ana rekebisha.

Nakumbuka kipindi cha nyuma enzi za maigizo ya Tausi, Mambo hayo na mchezo wa mzee majuto tulikuwa tunaenda kwake tupo wadogo darasa la 3-5 kwa ajili ya TV. Ila shangazi alikuwa tukienda anatuletea ukauzu, wale ndugu zake wanafujo utakuta labda apple wamekula wao utaambiwa ww basi unakuwa mpole.

Nakumbuka kipindi cha nyuma bibi alienda kumtizama mama yetu mdogo anaumwa, ila bibi kidogo ana matatizo ya miguu, babu akamwambia mama yako kaenda mtizama mdogo wake, akirudi mrudishe na gari hilo. Mjomba akamjibu "nampeleka mama mkwe beach......",hii kauli ili mkela babu na kweli bibi alitembea na miguu mpaka kituoni kagombania gari ,kafika usiku babu alimaind kishenzi. Akamchana akamwambia husitegemee mimi kutia mguu nyumabani kwako na mjomba hapa Dar ana nyumba kama 10. Kutokana na tabia za uchoyo na roho mbaya ya mke wake plus kauli ya babu, hamna ndugu aliyekuwa akifikia kwake wala kwenda kumtembelea .

Sasa anakaribia kustaff analamika sana kwanini hatumtembelei, kuna siku alinisema "siku hizi unitembelei kama zamani......" nikaa kimya siku mjibu sababu ni mjomba wangu na muheshim ila tatizo la mke wake analijua na kumbuka mara mwisho kwenda kwake nipo darasa la tano nikaenda tena kipindi nipo form 6 kumpelekea barua yake kutoka kwa mjomba yetu mkubwa,baada ya hapo nikaenda mwaka juzi kwenye sherehe ya mwanae basi na mpaka sasa sijatia mguu.
 
Bila wanawake hii dunia ingekuwa sehemu salama tatizo ni namna tu ya kuendeleza kizazi ila wanawake ni viumbe wa ajabu sana.
 
Nakerwa zaidi na tabia za baadhi ya wake kuwachukia mama wa waume zao. Mtu kapambana na mtoto mpaka hapo mlipokutana alaf kisa amekupata basi ndo akate mazoea na mama yake! Kijana akimjali mama yake kidogo basi mke full kutafuta njia za kuwafarakisha, Hasa mwanamke ambae tayari mmezaa ndo wanadharau zaid wakwe zao wakike, Mungu atusaidie!
 
Nipo mkoa Fulani kanda ya ziwa kikazi nilihamishiwa huku kwa bahati nzuri huku nilimkuta ndugu yangu mmoja tunaelewana Sana maana tumekua wote enzi hizo.

👇

Ndugu, usiingilie mambo ya mtu na mkewe. Mwisho wa siku wewe ndio utaonekana mbaya. Kama rafiki yako haoni tatizo, tambaa. Miaka yote si umesavaivu bila kampani ya jamaa yako?
 
Back
Top Bottom