Wanawake (Mabinti) wanaovuta sigara

Wanawake (Mabinti) wanaovuta sigara

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Wakuu, naona kama hii kitu inaongezeka kwa kasi, kuna Wadada siku hizi wanapiga fegi (sigara) bila uoga kabisa.

Hatari ya Wanawake kuvuta sigara ni kubwa kuliko wanaume.

Kuna sehemu nimekaa hapa kuna mabinti wanne, wawili wabongo na wengine wazungu wapiga fegi unstoppable.

Na kila mwanamke anayevuta sigara lazima anakuwa amechora Tatoo kwenye sehemu moja wapo ya mwili wake, kuna uhusiano wowote ule wa Tatoo na kuvuta sigara?
 
Dah, hayo ni maisha binafsi ya watu jomba. Mwanaume mzima unakuwa mbea mbea.

Hizo ni roho chafu wanahitaji kuombewa sio kusengenywa.
Umeandika nini sasa?

Anyway inawezekana ndio mwisho wa fikra zako.
 
Matokeo ya kuiga tu mkuu wala sio kingine, tumeamua kuiga kila kitu na ndio tumefikia hapa.

Wadada wakigiriki, Croatia, warusi nk wanakula fegi sio poa.
 
Kila starehe ina athari mbaya zaidi kwa mwanamke kuliko mwanaume. Tumeshtuka!
 
Matokeo ya kuiga tu mkuu wala sio kingine, tumeamua kuiga kila kitu na ndio tumefikia hapa.

Wadada wakigiriki, Croatia, warusi nk wanakula fegi sio poa..
Aisee.
Madhara ya utandawazi
 
Unataka kusemaje
Naunga mkono hoja yake.

Mwanamke ana madhara zaidi katika jamii kuliko Mwanaume.

Akishiriki anasa yoyote impact yake ni kubwa kuliko ambavyo angeshiriki Mwanaume.

Ukitaka kupima kutakana na Mwanamke aliyezamia kwenye Pombe
 
Ni janga kwa kweli, nasio sigara tu, bangi na pombe navyo ndio hatari zaidi. % yao ya matumizi ya hivi vitu inakua kwa kasi sana, kinachouma zaidi unakuta vitoto vya kike vidogo sana vinavuta mabangi
 
Hapo Moshi shisha inataradadi kwa fujo.

Mkuu mimi hua nafurahi sana nikiona mwanamke mwenye alama zifuatazo;
1. Tatoo
2. Vipini puani, masikioni nk
3. Mvuta fegi hadharani
4. Vikuku miguuni.
Hivyo kwangu huwa ni vielelezo kwamba KAA MBALI! Kwahiyo nikiona wa aina hiyo wala sijisumbui najua tu hapo hamna mtu.
 
Back
Top Bottom