Wanawake majasiri kwenye biashara

Wanawake majasiri kwenye biashara

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
337
Reaction score
296
Imetoka kwenye gazeti la Rising Kashmir


KASHMIR kwa sasa inashuhudia idadi kubwa ya vijana wa kike wakiingia katika biasharaa ya ujasiriamali baada ya kuushinda uhafidhina, ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira

Kwa sasa wanawake wanatawala sekta za biashara ambazo kijadi zilikuwa na mwelekeo wa kufanywa na wanaume,na mara nyingi wanawake hao wamewashinda wenzao wa kiume kwa kuonyesha ujuzi wa hali ya juu wa kusimamia biashara hizo

Mwandishi wa makala ya Rising Kashmir Saba Khan alizungumza na wajasiriamali wanawake ambao, licha ya kukabiliwa na vikwazo, waliamua kufuata mapenzi yao na wanaendesha biashara zenye mafanikio.

Shameema Akhtar

Anayetokea eneo la Nagam wilayani Kulgam, Shahmeena Akhtar anaendesha duka la muda. Alianza ubia huu baada ya majukumu ya kulea familia yenye watoto 6 kumuelemea mabegani mwake "Nilikuwa na majukumu mengi begani na nina watoto 6. Ndiyo maana nilichukua hatua hii,”alisema Akhtar wakati akizungumzia safari yake.

Alisema, "Tulikuwa na mume wangu huko Delhi kutokana na hali yake ya afya, nilianza kufanya kazi huko. Nilipiga pasi nguo na kusaidia kaya nyingine katika kazi zao za nyumbani ili kupata pesa.”

Anaongeza kuwa hakuridhika kamwe na mishahara hiyo na baadaye waliporudi kutoka Delhi mwaka wa 2018, ndipo aliposikia juu ya mpango wa National Rural Livelihood Mission's (NRLM) UMEED.

Anasema alijiunga na mpango huo hali iliyomsaidia kupata mkopo wa kifedha kwa ajili ya biashara.

Nchini India Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo Vijijini, inaangazia kukuza mifumo ya kujiajiri na kupanga watu wa vijijini, haswa masikini.

Wazo la msingi la programu hii ni kuwapanga maskini katika Vikundi vya Kujisaidia (SHGs) na kuwafanya wawe na uwezo wa kujiajiri.

Huko Jammu na Kashmir, programu hii inaendeshwa kama Misheni ya Kijijini ya Jimbo la Jammu-Kashmir (JKSRLM).

Katika mahojiano hayo Akhtar alisema, "Mume wangu hakuwa mzima kwa hivyo hakuweza kutusaidia sana hivyo nikamwambia asiwe na wasiwasi nitashughulikia kila kitu."

Anasema Siku zote alitamani kufanya kitu cha kipekee lakini kwa sababu ya hali ya kifedha hakuweza kupokea msaada wowote.

"Mwanzoni kila mtu aliyesikia juu ya mtazamo wangu kuhusu kibiashara alinikatisha tamaa lakini hali hiyo ilikuwa ni sehemu ya safari na sasa kila mtu ananithamini."anasema Akhtar.

Anaamini kuwa wanawake hawapaswi kamwe kutegemea wengine, badala yake wanapaswa kusimama peke yao.

Khairulnissa

Khairulnissa binti mwenye umri wa miaka 23, anayetokea eneo la Hanji Khello wilayani Pulwama, anafanya biashara ya maziwa na pia anauza lishe ya ng'ombe.

Anaeleza alianza biashara yake baada ya kushindwa kutatua matatizo yaliyokuwa yakimkabili kutokana na ukosefu wa fedha Mnamo 2016 nilianza biashara yangu kwa msaada wa NRLM na walinipa msaada wa kifedha ambao niliweza kuanzisha biashara yangu.

Kwa sasa akiwa na usaidizi wa wafanyakazi wake sita anaweza kusambaza maziwa katika vijiji mbalimbali, ikiwemo Jammu Kashmir Milk Producers Cooperative Limited.

Akirejea kumbukumbu zake za utotoni, alisema, “Sikuzote nilitaka kuwa mfanyakazi wa serikali lakini leo nimegundua kwamba biashara ni bora zaidi kuliko kazi.”

Nilianza biashara yangu kutoka rupia 10,000 kwa msaada wa JKLRM na leo nimefikia nafasi ambayo ninafanya kazi kwa masaa 4 tu kwa siku na kupata pesa nzuri, anasema.

Anawasihi vijana wasisubiri ajira badala yake wajikite kuanzisha biashara

Asmat Ara

Mwanamke Mwingine mjasiriamali,Asmat Ara mwenye umri wa miaka 25 kutoka wilaya ya Baramulla Kaskazini mwa Kashmir pamoja na dada zake wanaendesha duka linaloitwa Bismillah Copper- ambapo wanauza bidhaa za shaba.

"Kabla ya kuanza safari hii, tulikabiliwa na matatizo mengi. Tuliacha hata masomo yetu kutokana na hali mbaya ya kifedha. Lakini, sasa tumeanza tena masomo yetu kwa njia ya masafa,” alisema.

Alipouliza jinsi alivyoanza biashara hiyo, alisema, "kwa msaada wa mpango wa UMEED, nilianza biashara yangu na ninashukuru sana kwa msaada wao."

Mnamo 2014, nilitengeneza vyombo nyumbani ambavyo tulitengeneza maumbo na ukubwa tofauti wa vyombo kwa niaba ya wauzaji duka wengine na tukapata mishahara yetu, Ara alisema.

Anasema , mnamo 2016, alianzisha biashara yake mwenyewe ambapo Asmat na dada zake walitengeneza vyombo kwenye karakana yao na kuviuza kwenye duka lao.

Pia huchukua oda ya kutengeneza vyombo kulingana na mahitaji ya wateja.

"Tulikabiliwa na ukosoaji mwingi kwa kazi yetu. Kila mtu alitukatisha tamaa na kutuambia ni kazi ya wanaume, na kuwa wanawake tunawezaje kufanya biashara hiyo.

Hatukusikia," alisema na kuongeza "Kujitolea kwetu kwa kazi yetu ndio nguvu kubwa kwetu ndio maana tumefanikiwa leo." Ara anaendesha biashara yake kwa mafanikio na sasa ana watu 11 wanaofanya kazi katika kitengo chake cha biashara.

“Familia yangu ina furaha sana leo. Hata kijijini kwetu kila mtu anatuthamini na kuwaambia wengine wajifunze kutokana na safari yetu,” alisema na kuongeza “Ninashukuru sana JKRLM kwa sababu ilibadilisha maisha yetu.”

Madhu Bhala

Madhu Bhala, mkazi wa kijiji cha Nihalki huko Samba, anaendesha ufugaji wa kuku tangu 2010.“Mwanzoni mwa biashara yangu, nilikuwa na kuku 200 pekee na nilipata kidogo sana kwa sababu uwekezaji ulikuwa mdogo.

Mapato haya hayangeweza kutimiza mahitaji ya familia yangu,” alisema. Baadaye, mwaka 2018, aliingia katika mpango wa Umeed na akachukua usaidizi wa kifedha na kupanua biashara yake kwa kuanzisha shamba la kuku.

Akiongea na Maduhu kuhusu usaidizi wa familia yake, alisema mumewe amekuwa akimuunga mkono kila mara.

"Yeye ndiye nguzo yangu na kwa msaada wake nimefika hadi sasa," Bhala alisema.

Kwa sasa Madhu Bala husambaza kuku katika maeneo mbalimbali na kupata rupia 30,000 hadi 40,000 kwa mwezi kutokana na ufugaji wa kuku.

Anaamini kwamba ikiwa mtu ana nia ya kufikia malengo ya kitu chochote atoka katika eneo alilopo na kuchukua hatua ili kufikia lengo lake.
 
Nawapa kongole hao wanawake wamefanya Jambo zuri Sana....naamini kabisa itaongeza hamasa Kwa wanawake wengine duniani
 
Back
Top Bottom