Wanawake maoni katika hili suala

Wanawake maoni katika hili suala

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
311
Reaction score
326
Kutongoza ndio msingi wa mahusiano na ndoa. Mahusiano mengi kama sio yote huanza kwa mwanamke kutongozwa kisha huamua akubali ama akatae. Mara nyingi mwanamke ndiye anaeamua kama haya mahusiano yaanze ama yasianze.

Namna unavyomtongoza mwanamke inaweza kupelekea kukataa ama kukubali. Japo kuna mambo mengi ya kuzungumziwa katika hilo ila mie nitazungumzia jambo dogo sana na naomba wanawake mlioko JF mnipe maoni yenu.

Binafsi kwa uzoefu wangu nimeshatongoza wanawake kadhaa. Katika hao niliowatongoza niliwai kumbana na mkanganyiko fulani.

Baadhi ya Wanawake wanapenda kutongozwa kwa maneno 'mengi' yaani umuelezee mambo chungu nzima kabla hajakukubali na ukienda straight na kuwa short and clear UNAMKOSA, hawapendi useme tu "nakupenda, nataka kufunga ndoa nawe". Lakini kuna wanawake wengine akikuona maneno mengi sana ujue nae UMEMKOSA, hawa ni wanawake ambao huwa hawataki maneno mengi, wanatarajia uwe short & clear. Huwa wana mtazamo kuwa mwanaume anaongea sana ni MLAGHAI na mhuni tu.

Sasa mimi nimekuja hapa kutafuta general rule. Ipi kati ya hizo mbili huwa inapendwa sana. Wewe mwanamke funguka unapenda mtu akutongozeje mpaka uridhike na kwanini ? Unapenda maneno meengi au unataka ile direct to the point with just ONE sentence.
 
Ukiwa Maskini jiandae kutafuta nguvu za ziada na maneno ya ulaghai ktk utongozaji.

Ukiwa na pesa , acha pesa ikusaidie kutongoza Mana wanawake wanashida Sana.
 
Back
Top Bottom