Wanawake mkipata wapenzi wapya punguzeni "show off" kwenye "status za WhatsApp"

Wanawake mkipata wapenzi wapya punguzeni "show off" kwenye "status za WhatsApp"

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Story iko hivi....

Nilikua na mpenzi wangu ambae tulidumu kwenye mahusiano kwa takribani miezi 6 lakini tulipishana tu Kiswahili kdg tu na nilijaribu kuzungumza nae lakini nikaona kama mwenzangu bado kanuna flani na wakati tunazungumza mimi nilikua nimesafiri kikazi kwa muda wa mwezi mmoja so hatukua mkoa mmoja kama kawaida.

Kuna siku niliingia wasap nikakuta kaweka DP ya mwanaume mwingine nikajua tu tayari ana mpenzi mpya au huenda alikua nae kabla hata hatujapishana kiswahili so alichokua anatafuta ni sababu tu ili awe free.Binafsi nilivyoona vile wala sikutaka kuhoji mana nilishajua nini kinaendelea.

Kwakua namba yake sikuifuta niliendelea kuona status zake za WhatsApp akimposti kwa kasi yule jamaa yake mpya.

Sasa chakushangaza jana yule manzi kanicheki kwa normal text na kuniuliza "Mapenzi na mimi yamekufa ?"

Mimi nikamuuliza kwanini unasema hivyo, akanijibu "Mana naona uko kimya kama vile hunijui" Nikamwambia sio kwamba nipo kimya ila nilishaona wewe tayari una mpenzi mpya sasa si vyema mimi kuanza kukutumia text au kukupigia mana nitakua nakuharibia mahusiano yako akanambia "Sipo nae" nikamuuliza kwanini akanambia "mkorofi na mimi ukorofi sipendi" Nikahisi tu mbali na ukorofi kuna jambo atakua ananificha na huenda jamaa kashakula tunda kaona hakuna cha ziada.

Wanawake mnapoingia kwenye mahusiano mapya punguzeni show off za social media mana huwezi jua huenda huyo unaemtambia kwamba upo na mpenzi mpya siku moja ukahitaji support yake.

Na sisi wanaume tunajijua, tukiwa bado hatujakuvua nguo ya ndani huwa tunaonesha kujari asilimia 100%, ukiomba elfu 20,000 utashangaa unapewa 50,000 yani hiyo ni technic tu ya kukujaza upepo ila ukishatoa tunda tu hakuna rangi utaacha kuona otherwise upate bahati uolewe kweli.

Hakikisha kama unamposti mtu kwenye social media uwe na uhakika nae kwamba mnaenda kuingia kwenye ndoa mana siku ukiacha kumposti ni rahisi watu kujua kwamba mahusiano yako yapo kwenye hali gani.
 
Ila sijui unazungumzia wanawake wa wapi.. mashost zangu sionagi wakipost mabwana zao aisee.

Kuna mmoja pekee alikuwa anaweka Insta story.. huyu anaweka sbb ya uzungu aliokopi huko alipo kwa sasa
Ni kiashiria moja wapo upo na miaka zaidi ya 25 kuanzia huko watu hawanaga muda na hayo mambo 😂😂

Twazungumzia mabinti chibi ya 25
 
Mimi demu wangu akiniambia nimpost hua na hide wote namuacha yetetu

Alafu namba mbili ni hii 👇👇
b9528306be4e48e2ba02630f61a7e13c.jpg
 
Kisa kapata penzi jipya utu wangu akavua siku wakija kuachana thamani yangu ataijua niko busy. Haka kanyimbo kana maana kubwa hebu kuwa busy hata kama utampa nafasi usimpe kama ulivyompa mwanzo huenda akaja kuumiza tena baadae
 
Back
Top Bottom