Wanawake mlio kwenye ndoa badilikeni, mnachokifanya mnadhalilisha sana waume zenu.

Wanawake mlio kwenye ndoa badilikeni, mnachokifanya mnadhalilisha sana waume zenu.

Ndoa za siku hizi kutiana ukichaa tu, wake zetu wana matatizo kweli, hata ukiwafikisha wataibua matatizo mengine tu.
Mmeambiwa msilalamike kuhusu wake zenu maana they are image of you, so ukiona ana matatizo ujue 'kichwa cha familia' ndio kiko hivyo.
 
Mkuu Sasa Basi umegusa ukweli wanawake wenye tabia hiyo lazima mapovu yawatoke lakini ukweli umewapa hawajui kuwa hata sisi tunaodharaulika kwenye ndoa zetu huko nje tunasifiwa na kupewa vitu adim Ukisema cha nini mwenzio unasema nitakipata lini inabidi wajiongeze kiakili
Ushasema huko nje, huko nje unadhani shida yake ni nini? Lazima usifiwe hadi ujikute CR kumbe manfongo.
 
Atakuwa ni mke wangu huyo, hata hayo maneno yananigusa moja kwa zote.

Michaelray: We siasa basi kwa nini mke wangu kukuelezea mambo ya nyumba yangu?

Siasa Basi: Shikamoo mueshimiwa!!
Michaelray: Embu ntolee upuuzi Mimi, unajua nimemtoa wapi huyo Mke no.2.

Siasa Basi: Kaja mwenyewe kunielezea..
Michaelray: kukuelezea nini? (Akimkatisha).

Siasa Basi; Eti unakibamia(kwa sauti ya mnong'ono)
Michaelray: Ati Kibamia!! Mungu wangu. (Haya ikiwa imeufunika Uso wake)

Siasa Basi: Tena eti unapiga kibao kimoja kama yule jogoo pale( Anamwonyesha jogoo anayempanda mtetea aliyekaribu yao).

Michaelray: (hasemi kitu zaidi ya kuahusha pumzi kama Kobe Mzee).

Siasa Basi: Mzee nakushauri uache mapenzi na ndoa kwa kwa ujumla. Ujiite MAPENZI BASI.

Wanashikana Masharti, Onyesho linaisha jukwaani, Wanajamii Foramu wanashangilia wote isipokuwa Wenye Vibamia.

Karibu katika onyesho lijalo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] umenivunja mbavu zangu mkuu, kwamba sasa uitwe "Mapenzi basi"
 
Mmeambiwa msilalamike kuhusu wake zenu maana they are image of you, so ukiona ana matatizo ujue 'kichwa cha familia' ndio kiko hivyo.
Atoto katika ubora wako, haya bhana
 
Sio kweli maana yake kama wewe unavyomsifia wa nje na ndio ilivyo wa ndani hua anaonekana hana maana kawa wake zetu huwa hawatusifii hata ufanyaje
 
Mzigo mkubwa wa maisha huwaelemea zaidi wanaume kwa vile wao ndio wanaowajibika kuzitunza familia zao. Lakini kwa bahati mbaya sana wamekosa wake wakuwapa maneno mazuri ya kumfariji na kumuongezea matumaini, ili apumzike na kuburudika, zaidi anamuongezea shinikizo la damu, wasiwasi, msongo wa mawazo, mwisho anakosa hata hamu ya tendo la ndoa. Mke kutwa kulalamika, kunung'unika, kiburi na dharau.
 
Siku zote mwanamke hupenda shortcut ktk kutatua tatizo.
Na hayupo tayari kuongea na muhisika bora akalizungumze na watu wengine baki na siyo mhusika.
Yupo radhi acheat, na akikamatwa akaachwa anaanza kumlaumu mume wake kwa kumuacha na anaona km anaonewa
Hapa ndiyo huwa nashindwa kuwaelewa wanawake.

Stop: generazation!!
 
Mzigo mkubwa wa maisha huwaelemea zaidi wanaume kwa vile wao ndio wanaowajibika kuzitunza familia zao. Lakini kwa bahati mbaya sana wamekosa wake wakuwapa maneno mazuri ya kumfariji na kumuongezea matumaini, ili apumzike na kuburudika, zaidi anamuongezea shinikizo la damu, wasiwasi, msongo wa mawazo, mwisho anakosa hata hamu ya tendo la ndoa. Mke kutwa kulalamika, kunung'unika, kiburi na dharau.
Ni kweli kabisa, ndio maana hata life span yenu inazidi kupungua.
Tutajirekebisha na kuwafanya msijutie kuwa nasi, ila nanyi mkitulize.
 
Sio kweli maana yake kama wewe unavyomsifia wa nje na ndio ilivyo wa ndani hua anaonekana hana maana kawa wake zetu huwa hawatusifii hata ufanyaje
Tabia ya wanawake ya kulalamika, kunung'unika na kudeka inawaudhi wanaume wengi. Wamekaa kuwasema waume zao vibaya mbele za watu. Wanatia aibu tupu , ndio maana wamekuwa wepesi sana, ukimgusa tu tayari.
 
Ni kweli kabisa, ndio maana hata life span yenu inazidi kupungua.
Tutajirekebisha na kuwafanya msijutie kuwa nasi, ila nanyi mkitulize.
Safi sana atoto , unajua kumheshimu mume wako haina maana kujidhalilisha, kumuheshimu mume ni njia mojawapo tu ya kuonyesha upendo wako kwake na kuonyesha kuwa unamjali. Jukumu la mwanamke ni kumtunza na kumlimda mwanaume. Ukionyesha upendo wa kweli kwa mumeo, basi mumeo atakuwa tayari hata kujitolea muhanga kwa ajili yako. Sasa unakuta mke wakati wote limefura utazani limemeza chura, furaha ndani hakuna, ugomvi kila wakati, hapo nguvu ya kiume itatoka wapi.
 
Siasa basi, kuna wanawake wanawaheshimu waume zao acha kabisa, ila ndio wanakutana na waume vimeo wasiojali wala kuthamini.
Life isnt fair, unakuta mwanamke wa maana anakutana na gume gume hatari na kinyume chake pia.

Tujifunze tu kuthamini vile tulivyo navyo, tuchukuliane tu maana hakuna mkamilifu.
 
Unaonekana ni mshauri wa ndoa mzuri.. Ngoja na mm nakuja na matatizo yangu unitatulie
 
Back
Top Bottom