Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Wewe hunywagi mdada?Kwani nyie mkikaa baa pesa ngapi mnazicha kwa siku
Leo hii nywele tu siku mbili tatu kufumuliwa unaona hasara acheni ubinafsi wanaume
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe hunywagi mdada?Kwani nyie mkikaa baa pesa ngapi mnazicha kwa siku
Leo hii nywele tu siku mbili tatu kufumuliwa unaona hasara acheni ubinafsi wanaume
Hata siku tano au saba siku moja tu kuna siku nilitamani nilie kiukweli nimeombwa hela ya kusuka yaani kasukwa karibia siku mbili kakaanazo siku moja tu kafumua nilimwambia kuanzia Leo tusiombane hela za kusuka wala saloonKwani huwa zinakaa siku ngap kichwani
Usiwe mwepesi kukasirika na kujutia hela uliyotoa.
Hapo kuna ujumbe unapewa indirect.... Kuwa mwanaume hakikisha unajua nini sababu.
Kwa haraka haraka yaweza kuwa kuna kitu umemuudhi sasa hasira yake anaona Hata nywele ulizolipia ni kero. Kumbuka wanawake ni wabahili sana kufumua nywele hadi huwa zinavundia kichwani ( nawasomaga mnavolalamikia mawigi ya wake zenu).
Kama hujamuudhi wewe basi kuna shosti au ndugu yake kamwambia hizo nywele ni mbaya zimekufanya umekuwa kama chakubimbi..... Basi huko alikoenda kusuka hatorudi tena na atazifumua tuu hata kama aliyemwambia alitania.
Kuna dada mmoja alifika kazini jumatatu kasuka wivingi la bambucha, ukiongeza na mekapu alizokoleza usoni, kila mfanyakazi mwenzie alimwambia lake. Kijanammoja akamwambia yaani Salome, hizo nywele kama fagio la chelewa.... Wafanyakazi wengine wakacheka kwanguvu kama utani siku ikaisha.
Kesho yake Salome alifika kazini nywele zimefumuliwa.
Mwisho yawezakuwa msusi alimvuta sana hadi mishipa ya kichwa ikasinama... (Hapa ndo naelewa wanaume wakilalamika kuwa ikisimama muda mrefu wanaumia hehehee).
Mwisho kabisa kama uliona amependeza ila hukumsifia kwa kumwambia basi amejua hujazipenda.
Ubongo wa wanawake unafanya kazi tofauti na kwa namna yake, yahitaji Kuwa mdadisi sana kabla hujafanya maamuzi.
Na akiwa ni mdada anayejali pesa yako, atakaa hata miezi miwili bila kuomba hela ya kusuka, kufidia kuwa angekaa na hizo nywele muda huo kisha aombe hela nyingine ya kusukia.