Wanawake mna roho mbaya kama nini, ah!

Wanawake mna roho mbaya kama nini, ah!

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
475
Reaction score
353
Yaani kadada kamemset mzee (uncle wake wife) mpaka amekuwa kama zezeta. Picha kamili ipo hivi. Huyu ni mzee wa heshima kabisa, ni bosi wa taasisi moja nyeti hapa Dar. Siku moja hivi kama mwaka umepita huyo mzee alisepa home, akawa hajulikani alipo. Baadae tukasikia amepanga nyumba sehemu hapahapa Dar anaishi na mwanamke, (yaani kaacha nyumba yake ya kama 600 million, mke waliyeishi wote kama 20 yrs hivi, mtoto mmoja aged 20 na gari 2 ndogo). Huyo mke mpya akawa karibu na ndugu wa mwanaume mpaka alipopata uhakika kwamba mzee harudi tena nyumbani kwake. Akaanza kutimua ndugu mmoja mmoja mpaka akabaki yeye na mdingi tu. Kapewa mtaji anapiga dili za kwenda China kufuata bidhaa. Akisafiri anamwita mamake ndo aje akae na mumewe, ati hataki kumwacha na mtu mwingine. Sijui wanamlisha nini. Mdingi wa watu, yaani ukimwona kama msukule. Yupoyupo tu. Juzijuzi kulikuwa na shughuli ya kiukoo ndugu wakaamua kufanyia kwake, u know what? Eti huyo mother house kafunga vyumba vyote kaacha kimoja tu wazi kwamba wageni wote wa mumewe (wa kike na kiume) watumie hicho, ambacho mdogo wa mumewe amefikia humo! Halafu ndugu zake yeye wote wawili wa kike watumie vyumba 2 vilivyo empty. Walipolalamika, mama (huyo mdada sasa, ambae ni mdogo kwa my wife) kaja juu kishenzi, kwamba amefunga vyumba vingine kwa sababu last week aliibiwa pea ya viatu. Mdingi yupo kimya kama kamwagiwa mtaji, mkewe anadhalilisha ndugu zake wapatao 15, wawili kati yao ni wakubwa zake kisa pea ya viatu sijui vya 50,000. Mshahara wa huyu mzee ni kama 6 million per month. Utu wa mtu kwa pea ya viatu!!!!! Ndugu wakabeba mizigo yao hao wakasepa lakini wakaahidi hawatarudi tena. Mzee kampigia wife wangu simu kujaribu kureconcile (yeye ndio alianzisha kulalamika kuwa hawawezi kudhalilishwa na akataka kumchapa makofi mke wa uncle yake). Sasa mzee wa watu alichoongea hata hakieleweki, inaonekana ndugu anawapenda na dawa zimekolea. Wife hajui amsaidieje uncle wake wakati ndugu wengine wamemsusa mdingi, including mama yake mzazi!!! Tumsaidieje huyu mzee?? Wakati huohuo wadada acheni zenu bana!! Mnakuwaje na roho mbaya kuliko shetani? Ah!
 
Huwa siamini uchawi lakini hayo yashatokea kwa ndugu yangu wa karibu kabisa. Wataalam wanasema kuwa aliyewekewa dawa akivuka maji tu dawa inaisha nguvu. Ajaribu au tengenezeni mazingira ya huyo bwana kusafiri angalau kwenda zanzibar kwa ndege au hata kwa meli. Nadhani inaweza kusaidia.

Otherwise haujaeleza religional status zao, kama ni christian maombi yanatosha mwanamke alie ibiwa mume akisimama katika maombi na kushirikisha ndugu na jamaa mambo yote yatakuwa shwari kuu.
 
siku zote malipo ya uovu yanalipwa hapa hapa duniani. mzee kwa kupenda damu moto kamtelekeza mkewe wa ukweli. na sio bure kafanyiwa mambo...m 6 per month kadada kanazikamatia! anyway ushauri mzee apelekwe kwenye maombezi na amkabidhi Mungu maisha yake, baada ya hapo mzee aachane na kadada na arudi kwa mkewe wa ukweli amwombe radhi. otherwise huko mbele ya safari mzee ataanza kupangiwa zamu za kupika jikoni na kufua nguo za kadada na mama mkwe wa magumashi huku kadada kakiwa busy out na vijana wa damu moto kama yeye! mzee hawezi mikiki mikiki ya damu moto ktk 6by6!
 
Wasiliana na Zinduna atakusaidia. Kwa hapa jamvini nadhani yeye ndo mtaalamu wa hayo mambo ya uchawi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wale wote wabaya, Yatawakuta mabaya.
Aliacha mbachao kwa Msala upitao.
anatumikia adhabu ya kuitelekeza familia yake.

Ushauri:Atubu na amrudie Mungu na kurudi ktk familia yake yenye baraka za Mungu kwani naamini alifunga ndoa na huyo mke wa awali.
 
Hahaha, itakuwa Sumbawanga amu

subiri niende tena kule kuna mpaka radi na mvua ya kutengeneza maana hawa ...
Mdingi **** wenzako wanakula huku na huku akisafiri na nyumba anamwambia nunua vitu mletee na mwenzako.
Ila mke haambiwi hayo akisafiri peke yake vitu vinaanzia kwa nyumba ndogo kushushwa.
Akisafiri na mke ha ha ataenda kununua mdogo mtu aseme vya mkewe au gf wake kama si wifi mtu.
Fair play wote wanabiashara tena utakuwa nyumba ndogo anamjua mkubwa wala hana shida saa zingine wanagongana uchinani ila kila mtu kimpango wake.
We muite mkweo mueleweshe fairplay huyo si madawa ni ukichaa tu anauendekeza.
 
Last edited by a moderator:
Halafu kanamshawishi mzee aombe kustaafu apewe pension yake wafanye biashara za China wote.
 
Wanachokoseaga kwa watu kama hao wanatoaga siri zao zote ndio chanzo cha wadada kuwashika masikio hapo kazi ipo.
 
roho mbaya ya mwanamke iko wapi hapo?

Yaani mwanaume atafute kiranga chake asingizie roho mbaya ya mwanamke?

Kwanza alowaambia nyumba ndogo zina mapenzi na nyie ni nani?

Ujinga wa kumwacha mkeo mlotaabika nae ndo unawaponzaga....

Safi sana small hausi mkamue huyo baba mpaka atoke damu...... Iwe fundisho kwa wanaume wengine,[mjifunze kutulia kwenye ndoa zenu.......

Kamuaaa kamuuuua.........kamuuuuuuuaaaaaa na pension ikitoka kombaaaaaaaaa yoooooote
 
hahahahahah akamue babaaaaa kamuaaaaaaaaaaaaaaaa hahahahahahah
roho mbaya ya mwanamke iko wapi hapo?

Yaani mwanaume atafute kiranga chake asingizie roho mbaya ya mwanamke?

Kwanza alowaambia nyumba ndogo zina mapenzi na nyie ni nani?

Ujinga wa kumwacha mkeo mlotaabika nae ndo unawaponzaga....

Safi sana small hausi mkamue huyo baba mpaka atoke damu...... Iwe fundisho kwa wanaume wengine,[mjifunze kutulia kwenye ndoa zenu.......

Kamuaaa kamuuuua.........kamuuuuuuuaaaaaa na pension ikitoka kombaaaaaaaaa yoooooote
 
Wanawake wana roho mbaya sana
Cha msingi uyo mzee ni wa kufanyiwa maombi tuu mambo yatanyoka!
 
Back
Top Bottom