Wanawake mnajua muda mwingine mnakwaza?

Wanawake mnajua muda mwingine mnakwaza?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure[emoji2219][emoji2219]mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili,unapanga ndoa ya milioni 20

Wakati wewe mwenyewe hata hela ya suti unategemea uchangiwe acheni huu ujinga.Ukipanga shughuli angalia na mfuko wako acha mambo ya kuiga iga kisa umeona rafiki zako wamefanya sherehe ya kifahari.

Ishi maisha Yako na sio kuigaiga ndio maana wengi wenu hamuoi/hamuolewi[emoji2317]Unakaa na binti wa watu anakuambia anataka kwenye ndoa yake apande Range Rover wakati kwao uwani wamepaki ndala mbovu zilizotoboka, Shela unataka litoke Italy,Viatu vya Uturuki,Manukato ya Dubai,Suti ya Uingereza,

Wakati hata passport huna,umekazana kabisa mimi bila sherehe ya bajeti ya milioni 30 siolewi nyau wewe ungekuwa na misimamo hiyo si angekukuta na bikira yako[emoji706]Acheni kuwatesa vijana kihisia mnawalazimisha wafanye vitu vilivyo nje ya uwezo wao mwisho mnajikuta mnazalishwa na kuachwa.

Sio kila unachokiona kwenye vipindi vya CHEREKO CHEREKO na Ndoa Yako na wewe uviige.Chukua Bwana/Bibi Yako nenda kwa Pastor/Shehe/Mfungisha ndoa ukiwa na mashahidi wako na watu wachache maliza shughuli.

Unaalika watu 400 umekuwa serikali wewe kwamba umeitisha bunge?Kadi unapanga mchango laki unaijua laki ni asilimia ngapi ya mshahara wa mtu?Ukipanga jambo lako hakikisha asilimia 60

Kwenda juu unaitoa kwenye mfuko wako vinginevyo utakuja kulaumu watu bure.[emoji2317] nimeandika hapa kuna mtu kapanga sendoff ya milioni kumi kabakiza vikao vitano na michango mpaka sasa kapata laki nane anaishia kulaumu watu na ndugu tu[emoji2219][emoji2219][emoji2219]
 
.Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure[emoji2219][emoji2219]mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili,unapanga ndoa ya milioni 20
Natamani umwambie bf wang haya maneno, nshasema mm ya asubuh tu baada ya swala ya Fajr ndo imeisha, Ye anataka masherehe makubwa hvyo anataka ajipange had mwakani MJUSI huyu mxiuuu!
 
Ujinga tu kuangalia watu wanataka nini.
Maisha ya sasa yanachangamoto sana ,ukinzingatia na uchumi wa wengi ndio hivyo bora kujibana na kufanya ndogo tu hayo ni maisha yenu kuliko kuja kuja kuingia madeni ya ajabu ajabu furaha ya siku moja isikufanye ikuache na majuto
 
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure[emoji2219][emoji2219]mtu unapanga sendoff ya

Kwenda juu unaitoa kwenye mfuko wako vinginevyo utakuja kulaumu watu bure.[emoji2317] nimeandika hapa kuna mtu kapanga sendoff ya milioni kumi kabakiza vikao vitano na michango mpaka sasa kapata laki nane anaishia kulaumu watu na ndugu tu[emoji2219][emoji2219][emoji2219]

Pita kando kaka, linda nafsi yako tu
Mwache ajifie na upumbavu wake ..
Hapo anataka kulingishia mashosti zake tu halafu hata ndoa haiwazii.

People change when they want to..
No amount of coercion or seduction will enable people to change
 
Natamani umwambie bf wang haya maneno, nshasema mm ya asubuh tu baada ya swala ya Fajr ndo imeisha, Ye anataka masherehe makubwa hvyo anataka ajipange had mwakani MJUSI huyu mxiuuu!
Natamani ningeoa mke wa namn hii, ni ajabu mwanaume kupenda sherehe namna hiyo.
Mara nyingi wanaokuwaga na hamu na sherehe kubwa ni wanawake, huyo jamaa ako nae apimwe huyo labda kuna kingine anahofia.
 
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure[emoji2219][emoji2219]mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili,unapanga ndoa ya milioni 20
Acha tu. Kipindi hiki mtu akifanya sherehe kwa kutegemea michango anatafuta mikosi tu
 
Natamani ningeoa mke wa namn hii, ni ajabu mwanaume kupenda sherehe namna hiyo.
Mara nyingi wanaokuwaga na hamu na sherehe kubwa ni wanawake, huyo jamaa ako nae apimwe huyo labda kuna kingine anahofia.
si mwingine bali mama mzazi, maana anajitoa sana kwenye masherehe kwaio lazima atataka kurudishiwa fadhila, badala wafanye tenda wema nenda zako. Mi nawaangalia nikipata mwny mawazo ka yangu asije nilaum kwakweli
 
Hii tabia ya kupanga sherehe kwa kutegemea michango ya watu Ife mtakuja kununia watu bure[emoji2219][emoji2219]mtu unapanga sendoff ya milioni kumi wakati wewe mwenyewe huna hata uwezo wa kutoa milioni mbili,unapanga ndoa ya milioni 20

Umeongea ukweli kwa hisia na hasira kidogo
Kama anataka vitu asivyo afford yeye wala wewe, mwache! Mwache akutane na anayeweza kumpa maana havitaishia kwenye shela na gari ya harusi...... vitaendelea hadi kwenye maisha yenu ya kila siku

Unaweza kuja kumlaumu kumbe wa kulaumiwa ni wewe
KANYEGELO
 
si mwingine bali mama mzazi, maana anajitoa sana kwenye masherehe kwaio lazima atataka kurudishiwa fadhila, badala wafanye tenda wema nenda zako. Mi nawaangalia nikipata mwny mawazo ka yangu asije nilaum kwakweli
Ohooo kama ni mama apo kumshawishi akubaliane na wewe ni kazi sana. Lazma nae atataka achangiwe kama alivochanga.
 
Sendoff laki 8 ikiongezeka sana itafika 1.2,kwakuwashauri ni bora mkafanya sherehe moja yani sendoff+harusi kama tukio moja at least inawezapatikana hela yenye nguvu
 
Pita kando kaka, linda nafsi yako tu
Mwache ajifie na upumbavu wake ..
Hapo anataka kulingishia mashosti zake tu halafu hata ndoa haiwazii.

People change when they want to..
No amount of coercion or seduction will enable people to change

Maamuzi sahihi

Mke bora au mume bora ni yule anayeelewa uhalisia wa maisha na anayekusaidia kukusanya kile mlicho nacho kwaajili ya kuiboresha kesho yenu na sio yule anauetapanya bila kujua kesho itakuaje

Vijana fanyeni kisichowakwamisha kesho, kuna maisha baada ya harusi na sendoff.
 
Jitu lina harusi yake linanifosi eti niweke ahadi sh ngapi 🤔🤔haya mambo ya harusi sio lazima kujaza watu fanyeni kimya kimya
 
Kuna binti ananiforce hela ya kujitambulisha tu iwe zaidi ya laki 3,mimi nilikuwa naona 150,000 inatosha.

Ananiambia kama siwez andaa laki 3 ni bora asiwajulishe kaka zake,na aondoke kwangu.

Afu wakati huo n singo maza
 
Back
Top Bottom