una maana gani wanawake wanapovaaa?
au ulimaanisha wanapopendeza machono pako?
MAnake naona topic haina jibu moja, kama ailvyosema mmoja hapo juu.
Wanawake tunavaa kutegemeana na wakati, ila unavyotuona unajua mwenyewe, mimi mfano nikivaa suruale kwa kuwa nasafiri, sitaki bugudha ya sketi, wewe utaweza kuona nakutega, au ninapovaa hijabu utasema nakutega ili unfuatilie ndani nina nini,
Ila wanawake tunavaa ili
- kujisitiri na hali ya hewa na mazingira, mfano singlendi, sweater, suruale, nk
- kuweza kufanya shughuli inayotakiwa kwa ufanisi, mfano manesi, madereva, mafundi nk
- kuonyesha hisia za ndani mfano- niko kikazi zaidi, tafadhali niheshimu, tafadhali nunua hii bidhaa, tafadhali ona urembo wangu lakini niheshimu, usiniogope, japo mzuri sana lakini karibu, nk
Sasa wewe utaionaje singlendi yangu au hijabu yangu, kutokana na akili yako na umbo langu hilo swala jingine.