Wanawake mnazidi kujipoteza data

Wanawake mnazidi kujipoteza data

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Kuna wakati najiuliza maswali mengi nakosa majibu! Utofauti wa mwanamke na mwanaume upo na kila mtu anafahamu hilo, ila tunaamua kuchagua tu kuziba masikio na kusema kuwa tupo sawa.

Hii picha imenifanya nifikirie mbali sana, sikatai kuwa kuna maaskari game wanawake ila sio kila eneo la game unaweza kumpeleka mwanamke kufanya kazi.
1740926034904.jpg


Kupambana na majangili kwa mara zote huwa ni kazi ambayo inahitaji mtu asiye na huruma kwani kuna mawili kwenye mipambano hiyo, aidha jangili akutoe uhai au wewe umtoe uhai jangili.

Mara kadhaa pia tumepata kusikia kuwa kwenye hifadhi mbalimbali haswa ya Gombe, wanyama kama Nyani pamoja na Sokwe kuwa huwa hawana adabu mbele ya wanawake.

Leo ni siku nyingine ambayo inazidi kuwafanya wanawake wachache wajione wanaweza kubeba majukumu na nafasi za wanaume.

Enewei: kuna wanajeshi walienda vitani ila badala ya kurudi na ushindi wakarejea na mimba.
 
Siku ukikutana na Sokwe ndo utajua dharau pro max zilivyo
1740926858062.jpg
 
Back
Top Bottom