Wana Jf, nawashukuru sana kwa mawazo yenu katika kumsaida mwenzetu juu ya swali hilo. Kifupi, badala ya kuumiza sana vichwa, kwa nini tusitumie kanuni za Muumba wetu? Mke mmoja/mume mmoja tu!!! Simple. Mtamaliza butcher, nyama ni ile ile. Kwa nini dhamiri yako ibaki ikikushtaki??? Kuna faida gani kuvunja amri ya Mungu? Pima faida na hasara za kuvunja amri zake uone kipi BORA. Hivi usipotembea nje ya ndoa, huoni utakuwa na amani tele?
1. Dhamiri yako itakuwa safi mbele na Mungu na mbele ya mwenzi wako.
2. Ukipata kahoma hutaogopa "labda nimeukwaaa, labda,...n.k."
3. Kila mara hata simu yako ikipigwa huna wasiwasi 'Labda hawara nini, je, nikaongelee wapi mwenzangu asisikie??"
4. Pesa zako zitatumika kihalali tu, sbb hutahonga, hutaficha kipato chako, maana matumizi mkeo/mumeo atayajua na mtapanga pamoja.
5. Utaweka mfano bora kwa watoto wako, ambao wanaweza wakauiga katika ndoa zao zijazo.
6. Mapenzi yenu yatadumu milele, kuanzia katika maisha ya sasa na ya paradiso ijayo.
7. Kuaminiana ndani ya ndoa kutajengeka sana. Hofu ya mtoto mchanga kubemendwa haitakuwepo.
Jamani kifupi, moyo wa mtu una siri nyingi sana, nyepesi nyepesi na nzito kabisa, Utawaficha wanadamu, lakini Mungu HAFICHWI NG'O.
TAFAKARI.