Wanawake mtatuua kwa kibondo....kha!

Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2008
Posts
15,321
Reaction score
10,075
Bishanga nikichezea kichapo toka kwa mama Kayaii nikaja kulalamika hapa mmu mnanicheka,jamani zis is a serious problem,hebu someni hii toka front page ya 'daily news' ya leo:
Kenyan men urged to boycott meals in abuse protest:
A Kenyan men's lobby group has called for a six day food boycott to highlight what it says is increasing domestic violence against men......
Tufunguke jamani,tuchukue hatua, hawa wanawake watatuua kwa kibondo,ohoooooooooo!!!!! Mimi nimeanza mazoezi ya karate,wenzangu sijui mna plan nini.
 
Bana haya mambo ya aibu!Upigwe na mwanamke!Haiwezekani!
 
Saanyengine mkipigwa mnastahili sababu ya kujitia wapofu....

AF hivi unadhani masikhara? Wanawake wanatutandika kweli kweli,halafu usiombe kupigwa na mwanamke,hawana hata chembe ya huruma,ni boom boom kwa kwenda mbele utadhani anachanja kuni.
 
Ukioa mkurya itawezekana teh teh teh[/QUOTE)
nothing to do with tribes,ni hulka ya mtu tu,hata kwetu uhayani
Ni vibondo kwa kwenda mbele,njemba zinaficha tu kazi kusingizia wameanguka kwenye ngazi.
 
nyie mnashangaa,kuna mjeda fulani pale maeneo ya karakata alitimliwa kaz becouze of that,alikua anapigwa adhalani huku kavaa migwanda yake.
 
AF hivi unadhani masikhara? Wanawake wanatutandika kweli kweli,halafu usiombe kupigwa na mwanamke,hawana hata chembe ya huruma,ni boom boom kwa kwenda mbele utadhani anachanja kuni.
Lakini haiumi sana kama akikupiga mwanamme,simnajua nyie vp mnapiga manake kama una twanga mpunga hata huruma yakusema huyu mwanamke huenda jioni akanifanya nilale kwa raha walaaaaaaaaaaa ni ngumu na mateke kwa kwenda mbele mpaka jino linatoka sehemu yake.
 
nyie mnashangaa,kuna mjeda fulani pale maeneo ya karakata alitimliwa kaz becouze of that,alikua anapigwa adhalani huku kavaa migwanda yake.
unaona sasa mambo ya gender bias? Sasa kwa nini afukuzwe kazi kisa kupigwa na mkewe.Juzi kijana mmoja mfanyakazi wa benki kaburutwa na mkewe toka kaunta hadi chini pwaaaaa kidogo amtegue kiuno,mambo gani haya jamani?
 
all forms of domestic violence ni mbaya,mi nataka tu ku highlight hili tatizo la wanaume kupigwa na wake zao,tujue na kukubali kuwa lipo na ikiwezekana kama jamii tulifanyie kazi....mambo ya kusema 'mwache apigwe' yatasababisha vilema na hata vifo.
 
Jee wanaume kuwapiga wake zao ni sawa au mfanye nyie tuu? au mwanamke kaumbiwa kichapo...
 
Bishanga ukiangalia asilimia kubwa ya wanaume wanaopigwa na wake zao ni wanaume walevi. Ukiwa umelewa chakali lazima mwanamke akulambe makofi kwa sababu hata nguvu za kurusha ngumi hauna.
 
mkurya huyo!
Siyo rahisi mkurya mwanaume kubondwa na mwanamke, maana kati ya zana anazopewa mwanaume siku ya harusi na wazazi wake ni pamoja na sime na rungu kwa ajili ya kudumishia ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…