benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Wanawake wa Jimbo la Mufindi wamemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mitungi ya gesi ya kupikia, itakayowasaidia kuondokana na changamoto ya matumizi ya kuni na mikaa.
Kauli hiyo waliitoa jimboni humo juzi, Mbunge Kigahe aliwapokabidhi mitungi ya gesi 500 yenye thamani ya sh. milioni 50 iliyotolewa na Rais Samia. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mufindi, Frida Kahaya alimshukuru Rais Samia kwa kutoa mitungi hivo ikiwa ni sehemu ya nishati safi isiyo na athari kwa afya za wananchi.
Alisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa wanachama na wananchi wa Mufindi. Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu, Kata ya Ifwagi, wilayani humo, Magreth Kaguo, alisema Rais Samia amefanya jambo kubwa wilayani humo, lililoweka alama kwa wanawake.
Aliongeza suala hilo limegusa maisha ya wanawake wa Mufindi na kuendelea kumkumbuka Rais Samia kwa kumwombea heri katika ongozi wake.
"Tunamshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani amegusa maisha yetu, ameweka rekodi kubwa katika maisha yetu. Unapozungumzia maisha ya mwanamke wa kijijini kama sisi, huwezi kuacha kutaja suala la nishati ya kupikia, tunamshukuru sana na tunaendelea kumunga mkono, alisema.