Wanawake na kisirani cha ujumbe wa simu…………………..!

Wanawake na kisirani cha ujumbe wa simu…………………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Mwanaume anapotuma ujumbe wa simu kwa mpenzi wake, akimwambia kwamba, hataweza kutimiza ahadi ya kukutana naye jioni kama walivyokubaliana, kwa mwanamke tafsiri itakuwa nyingine. Wataalamu wa tofauti ya mawasiliano kati ya jinsia wanasema, mwanamke mara nyingi, tafsiri yake kwenye ujumbe wa simu ni tofauti na mwanaume. Kwa sababu ya kuishi kwa hisia na kugusika kirahisi zaidi, mwanamke hutafsiri kauli kama hii ya maandishi ya kutomudu kutimiza ahadi, vingine kabisa.

Mwanamke hutafsiri kwamba, ameambiwa, ‘nimepata mwanamke mwingine ambaye nadhani ndiye anayestahili kutoka nami jioni hii.' Hilo ndilo litakaloenda kwenye akili ya mwanamke, mara baada ya kupokea ujumbe wa maandishi. Siyo kwamba, atafikiria hivyo moja kwa moja, bali kuna kitu, huko nyuma kabisa ya ubongo, kitakuwa kinamwambia, huyo mwanaume ana mtu mwingine. Kwa mwanamke, kuna tofauti, kwani mwanamke huishi kwa hisia, hivyo, sauti kwake hufanya tofauti kubwa. Kuna wakati, ujumbe halali kabisa kutoka kwa mwanaume unaweza kutafsiriwa kwa njia ya ajabu sana na mwanamke.

Ujumbe wa maandishi kwa mwanamke unaonekana kama kitu kikavu sana, ndiyo maana unapata tafsiri isiyo sahihi. Wakati mwanaume anaona ni sawa tu kutuma ujumbe wa maandishi, mwanamke anajihisi vizuri kupigiwa au kupiga simu. Kusikia sauti kunamfanya ahisi ukaribu na hivyo uhakika wa uhusiano na mwanaume.
Na ndio maana ni rahisi kwa mwanamke kumpigia simu mpenzi wake, kuliko kumtumia ujumbe. Kwa mwanaume ujumbe na kupiga simu ni sawa tu. Mwanamke na mwanaume wanatofautiana kihisia.

Ukweli ni kwamba mwanamke hugusika kirahisi kuliko mwanaume, na hivyo, hupenda kukagua kila jambo au mwenendo wa mwanaume. Kwa hiyo kitu kama mawasiliano rahisi ya simu kimesaidia sana kupanua wigo wa maendeleao kwa njia mbalimbali, lakini, kwa pande mwingine kimewaletea wapenzi kisirani.
Inakuwa tamu na nzuri pale mwanamke anapopokea ujumbe usemao, ‘ninakupenda honey' au ‘tutaonana muda mfupi ujao' lakini, siyo anapopokea ujumbe usemao, ‘nitachelewa kurudi, kuna kazi za ziada.' Kama nilivyobainisha, wanaume hupenda kutuma ujumbe, kuliko kupiga simu, kwani hutaka kusema wanachotaka kusema, basi.

Lakini wanawake hupenda kuzungumza badala ya ujumbe. Kuzungumza huwapa hisia za ukaribu wa kihisia na hivyo kunapokosekana, ikatumika njia ya maandishi, huhisi kuwa ujumbe uliotumwa haukutiliwa maanani.
Badala ya kutuma ujumbe kusema, hataweza kutimiza ahadi, mwanaume angetakiwa kupiga simu. Hata kama hatakuwa kazini bali kwa hawara, akipiga simu, mashaka kwa mpenzi wake huwa madogo, kwani atahisi kujali, kuliko kama angetuma ujumbe. Wanawake wanapaswa kujua kwamba wanaume hawaamini sana katika hisia kama wanavyoamini wao.

Ndiyo maana siyo ajabu kwa mwanaume kutuma ujumbe wa simu kumjulisha mpenzi wake kwamba amefiwa na baba yake. Hapa mwanamke anaweza kushangaa sana kwamba, inakuwaje mtu afiwe na baba yake na amtumie ujumbe tu, badala ya kupiga. Hii ni sawa na taarifa ya kulala nje ya nyumbani.
Mwanaume anaweza kumtumia mkewe ujumbe wa simu kwamba, hataweza kurudi nyumbani kutokana na kazi za dharura ofisini, kwa mwanamke, jambo hili ni kubwa na lingepaswa kupigiwa simu ili wapenzi wazungumze. Kwake sauti ina maana ya kujali zaidi, hivyo kuonesha kwamba, mtu amelichukulia jambo kwa dhati. Kwa mwanaume, taarifa ni taarifa, bila kujali imetolewa vipi.
 
Mkuu leo ndio umenfumbua macho kuna chick alikuwa anazengua nikamtumia mesage kama amenichoka aniambie yeye akajibu bila kufikiri kumbe mwanaume nilshahamua kusepa.alvyonijibu kwa txt nikadhani anamaanisha kama mimi.nikamuaga kwa txt baada ya wiki c akarudi analalamika sikumpgia simu so akuamini mesage alitaka tuongee au tuonane face2face.nikamwambia maji yashamwgika kilichopo apge deki
 
Nadhani hii kitu ndiyo inatusumbua wengi!! Unafanya kitu ukidhania mwenzako atakuelewa kumbe ndo umechokoza moto!! Ahsante Mkuu kwa ujumbe na darasa zuri.
 
Naomba uedit pale kwenye mstari unaosema'' Mwanamke anaweza kumtumia ujembe mkewe'' ili usomeke vizuri mkuu
 
Mtambuzi acha wewe, mbona mie napenda msg kuliko kupigiwa?
tena akiniambia amebanwa huwezi kuja imekula kwake, maana napanga ratiba mpya, nitanuna tu kama akichelewa kuniarifu kuwa hawezi kuja, ila akiniarifu mapema kuwa ameahirisha uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii atanikuta movieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mtambuzi acha wewe, mbona mie napenda msg kuliko kupigiwa?
tena akiniambia amebanwa huwezi kuja imekula kwake, maana napanga ratiba mpya, nitanuna tu kama akichelewa kuniarifu kuwa hawezi kuja, ila akiniarifu mapema kuwa ameahirisha uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii atanikuta movieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Lakini kiroho kitakuwa kinakuuma kwa mbaaaali......................
 
Heshima yako baba,asa mbona malalamiko yangu kwa mkweo ndio umeyaanika hapa?!ila nashukuru coz alikuelewa na sasa anaipigia cm mpaka raha!
 
Heshima yako baba,asa mbona malalamiko yangu kwa mkweo ndio umeyaanika hapa?!ila nashukuru coz alikuelewa na sasa anaipigia cm mpaka raha!
Nilimshauri namna ya kuku-handle kwa makini, nashukuru kama amejirekebisha sasa....................
 
Back
Top Bottom