JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imewakamata jumla ya Wanawake na mabinti 16 wanaojihusisha na mtandao wa matendo maovu ikiwemo kuhamasisha ukahaba kwa kucheza ngoma za usiku maarufu kama 'Kibao Kata' bila staha.
Akizungumza kuhusu matukio hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Watu hao wamewakamata kutoka maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam yakiwemo, Mwananyamala, Kinondoni, Tandale, Sinza, Buza na Magomeni. Ameeleza kuwa watafikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria.
Naibu Waziri Sagini amesema idadi kubwa ya wanaojihusisha na matendo hayo ambayo ni kinyume cha sheria ni wanawake na mabinti wadogo wenye umri chini ya miaka 18 ambapo uchunguzi umebaini kuwa wanawake hao wanaoonekana kukubuhu kufanya vitendo hivyo husafirishwa kwenda ughaibuni na kutumikishwa katika biashara ya ukahaba, jambo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo litahakikisha linaendelea kudhibiti mitandao ya watu hao ikiwa ni pamoja na kuendeleza msako na utekelezaji wa maagizo mbalimbali yatakayotolewa katika maeneo yaliyotajwa kukamatwa watuhumiwa hao.