Wanawake na maradhi ya urembo inasikitisha sana

Wanawake na maradhi ya urembo inasikitisha sana

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.

Ama kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo,

Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.

Akizungumza na paparazi juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.

"Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.

"Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,"alisema Khadija.

Akaongeza: "Nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani," aliongeza.
Khadija Omar, mkazi wa Kigogo.
Khadija alisema kesho yake alikimbizwa Hospitali ya Amana, Dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

"Nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa Hospitali ya Macho ya CCBRT (Msasani, Dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo," aliongeza Khadija kwa majonzi.

Alisema kule CCBRT alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Jumapili iliyopita Khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.

Jumatatu iliyopita Khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.

Daktari mmoja wa CCBRT ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: "Khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu' iliyotumika.

Taarifa zaidi zinasema, Jane na Koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo Khadija walikamatwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MGN/RB/13021/2013.

Hii inaweza kuwa fundisho kwa kinadada wengi wa mjini wakiwemo mastaa wa filamu, muziki na mitindo ambao ni watumiaji wakubwa wa urembo huo unaodaiwa kuwa na madhara makubwa kwa mtumiaji yakiwemo hayo ya kuwa kipofu.

vicknyusi+no1.JPG
 
ishu hapa ni ignorance zaidi

sawa na wale wanatengeneza mkorogo huku hawajui ni sumu gani wanazi changanya
 
wanaukumbi.

ama kweli hujafa hujaumbika, mrembo khadija omar, mkazi wa kigogo, dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo,


tukio hilo lilitokea novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.
Akizungumza na paparazi juzi huku akimwaga machozi, khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.

“mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.
“muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,”alisema khadija.
Akaongeza: “nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani,” aliongeza.
Khadija omar, mkazi wa kigogo.
Khadija alisema kesho yake alikimbizwa hospitali ya amana, dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa hospitali ya macho ya ccbrt (msasani, dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo,” aliongeza khadija kwa majonzi.
Alisema kule ccbrt alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.

Baada ya zoezi hilo kufanyika, jumapili iliyopita khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.
Jumatatu iliyopita khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.
Daktari mmoja wa ccbrt ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: “khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu’ iliyotumika.
Taarifa zaidi zinasema, jane na koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo khadija walikamatwa na polisi wa kituo cha magomeni jijini dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba mgn/rb/13021/2013.

Hii inaweza kuwa fundisho kwa kinadada wengi wa mjini wakiwemo mastaa wa filamu, muziki na mitindo ambao ni watumiaji wakubwa wa urembo huo unaodaiwa kuwa na madhara makubwa kwa mtumiaji yakiwemo hayo ya kuwa kipofu.




ni vyema watu wakawa makini kwa kila hatua anayo ichukua.

Pengine ni ajali kama ajali nyingine lakini pengine zina epukika kabisa.

Pengine si kila fashion lazima tuzijue na hili ndilo lina tuponza wanadamu.

Hila bado najiuliza kweli hiyo gundi ni mahususi kwa kitukinacho kwenda kugusa mwili?


Ugua pole khadija.
 
Dah!"Supa glue"Hatukatai urembo kwa Dada zetu,ila kuweni makini sana na madhara yake.
 
Mambo ya kuiga ndiyo yanayowaponza, kwanza hizi salun za mtaani wengi wao hawana ujuzi wa vitu kope nchi zilizoendelea watu wa saluni wanasomea hiyo taaluma lakini huku hakuna hicho kitu ndio maana athari zinatokea
 
hiyo saluni ya uchochoroni sana wanatumia super glue ..ni hatari sana...hata hivo hizi kope sio kabisa kuanzia kuweka hadi kutoa ni matatizo ..mi nilishaapa sitaweka teeeena vitu hivi!!
 
Ye taratibu kwenye macho yake hakuwa nayo me ntaitoa wapi???[/QUO
mtu afanyaye kitu hakijui na kikamuathiri anastahili kuhurumiwa na kusaidiwa pale inapowezekana lakin kwa yule afanyae kitu akiwa anajua madhara yake na akaathrika hata uspomuonea huruma hapo sawa, inavyoonyesha huyo hajui madhara ya urembo wa kulazimisha
 
yaani hayo masihara na macho yangu uwa sipendi kabisa...
Too bad... so sad....
 
Mambo ya kuiga ndiyo yanayowaponza, kwanza hizi salun za mtaani wengi wao hawana ujuzi wa vitu kope nchi zilizoendelea watu wa saluni wanasomea hiyo taaluma lakini huku hakuna hicho kitu ndio maana athari zinatokea
Yaah umeongea point mzuri sana! By the way huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo hata siku moja.
Ila kinachotakiwa ni hawa dada zetu wahakikishe wanakwenda salon mzuri na inayotoa huduma mzuri na siyo bora salon.
Pia ni kweli salon za uswahilini wafanyakazi wao siyo maprofesional kama ilivyo kwa salon za kishua ila siyo salon zote za uswahilini ni mbaya au hawajui kazi…mteja mwenyewe ndiye aangalie ni salon gani ya kwenda na apate huduma mzuri
 
Pole yake.....Ah mim na hayo mavitu mbalimbali...
 
Back
Top Bottom