Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WANAWAKE NA UHURU
Anaandika, Robert Heriel
Nianze Kwa kuwapongeza Wanawake wote Duniani katika siku yenu hii. Ninyi ni Watu muhimu Sana ndani ya jamii. Na ili umuhimu wenu uwepo ni lazima muwe Huru. Na hicho ndicho leo ninaenda kukieleza Kwa UFUPI.
Mara Kwa mara nimekuwa nikionekana nikiwashambulia Wanawake, wengine imefika hatua ya kuniita Mchukia Wanawake, kwangu hilo sio tatizo kwani najua Watu wengi wanauelewa finyu Kwa sababu ya kutanguliza Mbele mihemko Yao.
Mwanamke lazima awe Huru ili aweze kuwa na umuhimu. Ili umfaidi Mwanamke na uone Raha ya kuishi na Mwanamke basi mpatie Uhuru.
Sisi kina Taikon, Watoto wa Tibeli hatuwezi ishi na mfungwa au mtumwa ndani ya nyumba moja. Hilo haliwezekani asilani,
Macho yetu yalishaona kuwa kuishi na mtu asiyehuru ni matatizo makubwa kuliko kuishi na mtu aliyehuru. Miongoni mwa matatizo na Mwanamke asiyehuru ni kutotabirika, Kutokana na Ku-Fake, unafiki, ku-pretend, jamii nyingi zinadhana isemayo Mwanamke ni kiumbe asiyeeleweka, hivi tangu lini mtu mfungwa na mtumwa aliyenyimwa Uhuru akaeleweka?
Mtu yeyote ambaye hayuko huru hawezi kujidhihirisha Tabia yake halisi NI ipi, ni mtu wa kuficha makucha, hata kama kitu hajapenda hatasema, au amechukia hatasema. Sasa MTU wa hivyo utanielewa?
Mwanamke anaweza kuigiza anakupenda au anakuheshimu ikiwa tuu hayupo huru, lakini akiwa huru hawezi kuigiza au ku-fake. Ni ngumu Sana MTU huru ku-fake.
Lakini Kabla mwanamke hajapewa Uhuru wake yapo maandalizi na mambo ya kuzingatia, mathalani
1. Kutoa Elimu na kubust Akili zao
Hapana Shaka Uhuru pasipo Elimu ni machafuko na maangamizo makubwa.
Huwezi mpa MTU mjinga Uhuru, lazima ataharibu.
Ni muhimu kuwa Wanawake Elimu ya kujitambua, Elimu ya dunia na mazingira, Elimu ya mahusiano, Elimu ya Mila na desturi inayohusu maadili ya jamii zao.
Kumpa Mwanamke Elimu njema ni kumpa Uhuru wa Akili.
Tunahitaji Elimu bora ya kumfanya Mwanamke awe Mwanamke, na sio Mwanamke atake kuwa mwanaume.
Ili Mwanamke awe huru lazima abaki kwenye nafasi ya uanamke,
2. Kupata ujuzi na kufanya kazi
Mwanamke akishapata Elimu kinachofuata ni kupewa ujuzi na kufanya kazi za uzalishaji Mali zinazolingana na Fikra na maumbile ya Kike ambazo hazitwezi utu wake. Mwanamke hawezi kuwa huru ikiwa atakuwa tegemezi.
Taikon huwaga nasemaga, dhana au sheria zinazohitaji Mwanamke kuhudumiwa zimelenga kumdhalilisha na kumnyanyasa Mwanamke. Kumfanya awe tegemezi Kwa Mwanaume.
Mwanamke kama MKE hahudumiwi kwani yeye ni sehemu ya Utawala, ni Msaidizi WA Mume, wote wanazalisha Mali, vikao wakaa pamoja, matatizo wanatatua pamoja iweje isemwe Mwanamke anahudumiwa.
Katika kupigania Uhuru WA Mwanamke, Sisi Watibeli Njia zetu zinaweza kuwa ngumu lakini ndio Njia thabiti na sahihi.
Ewe Binti yangu, epuka fikra za kuhudumiwa, fanya kazi. Tafuta mwanaume ambaye mtaunda serikali yenu, muwe kitu kimoja, yeye awe kichwa wewe uwe Mwili.
Mnapoanzisha familia epuka mambo haya:
i) Ubinafsi
Kauli za umimi na umiliki WA vitu ipigwe marufuku humo ndani.
Simu yangu, Gari yangu, nyumba yangu n.k. sio Rafiki kwenye familia.
Mshahara wangu, hakuna cha Mshahara wako ndani ya Familia.
Hakuna cha Mshahara wa Mke au wa mume, Mshahara wa familia yetu ni Tsh 1M
Bila kujali MKE au Mume kaingiza ngapi.
Kisha pangeni Bajeti, Mfano
1. Matumizi ya Nyumbani kama chakula, bills za umeme, maji, takataka, ulinzi, mawasiliano na usafiri n.k. laki laki nne.
2. Matumizi binafsi ya wanafamilia laki 200,000/=.
3. Wazazi 100,000/= (familia ya MKE 50,000/= familia ya Mume 50,000/=) hakuna cha kusema sijui mzazi wangu ni Bora au nini, ubinafsi huharibu Uhuru wa Familia na kukikosekana Uhuru basi uaminifu automatically unaondoka.
4. Akiba 100,000/=.
5. Zaka na Sadaka na misaada 100,000/=.
6. Mengineyo 100,000/=
Kipengele cha matumizi binafsi hapo ndio wengi wanakichanganya na Kuhudumiwa Kwa Mwanamke, hapo hakuna kuhudumiwa, hiyo ni Bajeti ya wanafamilia kulingana na matumizi ya kila mwanafamilia.
ii) Epuka kumdhulumu mwanafamilia
Iwe ni MKE au Mume au mtoto wako.
Ili familia iwe bora basi itakupasa utoe Haki, uwe mwenye Haki, kuwatendea wengine Haki hasa kwenye familia ni kujitendea mwenyewe Haki.
Vile unavyotaka kutendewa basi mtendee mwenzako.
Haki itahusu wajibu na Majukumu ya kila mwanafamilia.
iii) Msiachiane matatizo au misalaba
Kupeana majukumu sio kuachiana misalaba,
Kwa mfano serikali ya familia yenu imempa Mama jukumu la usafi WA nyumba na kuhakikisha nyumba, Watoto, na Mume wanakuwa Safi muda wote. Lakini unakuja kugundua kuwa MKE hatimizi jukumu hilo Kwa ufanisi.
Kama Baba ni lazima utake kujua ni Kwa nini Jambo hilo linatokea, fanya uchunguzi Kwa Siri, kisha ukipata majibu, ziba hayo mapengo, na sio kumsema na kumkaripia mkeo Kwa nguvu na kipigo.
Zingatia, usimhukumu Kwa ukali na ubaya MTU aliyefanya Jambo bila dhamiri(kukusudia). Unapobeba msalaba WA mwenza wako unabeba msalaba wako Mwenyewe, unapouangusha msalaba WA mwenza wako basi unaangusha msalaba wako Mwenyewe.
Mnaposaidizana Kwa pamoja kama mchwa mnajenga familia Bora na imara. Mfano sheria za familia yenu mmeamua impe jukumu kubwa mwanaume la kuzalisha Mali kwaajili ya familia, lakini wewe kama MKE unakuja kugundua kuwa Mumeo hatimizi huo wajibu Kwa ufanisi.
Usikimbilie kumtukana, kumkebehi na kumdharau, Angalia ni namna gani utamsaidia aweze kutimiza jukumu lake ili msikwame.
Kushirikiana na kuwa wamoja ni sehemu ya kumfanya Mwanamke kuwa Huru na kuyafurahia Maisha yake. Kwani atajiona naye anafaida ya kuishi Duniani.
Kutoshirikiana na kutomshirikisha Mkeo au kumzuia Mkeo asikusaidie katika matatizo na misalaba yako ni kujaribu kumkandamiza Uhuru wake.
3. Upendo
Mwanamke ili umpe Uhuru lazima uhakikishe anakupenda Sana.
Ni ngumu Sana kusalitiwa na Mwanamke anayekupenda.
Kama nitaulizwa Kati ya mwanaume na Mwanamke na Mwanaume Nani Msaliti basi nitasema Mwanaume ndiye Msaliti.
Mwanamke kukusaliti ni Long process hasa akiwa anakupenda kikamilifu,
Lakini Sisi wanaume kusaliti Wanawake ni Jambo Dogo Sana Kwa sababu tunaongozwa na tamaa ya Mwili.
Yaani Mwanamke akiamua ulale naye leoleo wala hatatumia nguvu nyingi bila kujali unampenda au haumpendi,
Lakini hauwezi kuamua kulala na Mwanamke mwenye MTU anayempenda leoleo yaani ndio umekutana naye.
Upendo unaambatana na uhuru
Mwanamke apewe Uhuru wa kuamua, kutenda lakini kutenda mambo mazuri. Wanawake ni viumbe wanaopenda kuongozwa Kwa upendo, na sio kufanywa watumwa.
Unapompa Uhuru Mwanamke kumbuka haimaanishi umemuachia Uhuru WA kujiongoza, hapana!
Mwanamke akijiongoza mwenyewe hujihisi hayupo salama, hujihisi hapendwi na kama hapendwi tafsiri yake hana thamani.
Mwanamke anahitaji Uhuru lakini anahitaji Uhuru WA kuongozwa na kuwa Chini ya Mwanaume anayempenda,
Mwanamke anapotaka kufanya Jambo Fulani baya huweza kufanya hivyo Kwa kutaka kukatazwa na MTU ampendaye.
Usipomkataza Mwanamke Jambo baya analotaka kulifanya ukamuachia Uhuru wake ataona haumpendi, kimsingi atakasirika Mno.
Lakini ni hatari kumkanya Mwanamke asiyekupenda kuacha Jambo Fulani, hata kama anajua ni Jambo Baya atazidisha Makusudically.
Elewa kuwa Wanawake hufanya mambo Yao kulingana na wale anaowapenda, yaani kama Mwanaume anayempenda anapenda Wanawake wavaa nguo Uchi, Mwanamke atavaa vivyohivyo ili kumfurahisha Mpenziwe.
Ukitaka kumbadilisha Mwanamke vyovyote utakavyo, basi itakupasa ujue huyo Mwanamke anampenda mwanaume yupi, kisha M-deal na huyo Mwanaume.
Taikon unataka kusemaje?
Nataka kusema hivi, Uhuru wa Mwanamke upo mikononi mwa Wanaume, hasa wale wanaowapenda.
Kitu pekee kitakachomfanya Mwanamke akukabidhi uhuru wake ni Upendo wake kwako na Imani yake kwako. Mambo hayo mawili lazima uhakikishe unayateka Kwa Mwanamke yeyote unayetaka awe Mkeo au mjenge familia wote.
Imani yake juu yako inatawaliwa na kiwango cha Uhuru utakaompa, Mwanamke anayekuficha mambo Kwa namna moja ama nyingine elewa kuwa kuna sehemu umekanyaga waya wa Uhuru wake.
Mwanamke hanaga kifua Kwa mtu anayempa Uhuru, atakuambia kila kitu ikiwa tuu atajiona salama mikononi mwako. Kama atakuona wewe ni sehemu ya Maisha yake, matatizo yake ni yako.
Lakini kama ni wale wazee wa kumkandia, kumkejeli hata Kwa Jambo Dogo tuu, hujuagi kumsifia hata afanye nini,
Jua hapo unakandamiza Uhuru wako.
Huyo atakuficha mambo mengi Mno.
Uhuru, Elimu au Haki Sawa havimfanyi Mwanamke kuwa Jeuri au Katili.
Isipokuwa Ujeuri na Kiburi Kwa Wanawake wengi chanzo chake ni manyanyaso, kukandamizwa, kuonewa na kuishi na Mwanaume asiyempenda.
Mwanamke kama hakupendi lazima akusumbue tuu fanya ufanyavyo, atakudharau hata kama unamlisha na kumhudumia, atakudhihaki na kutofuata amri na matakwa yako ikiwa hakupendi.
Elewa pia kuwa Mwanamke anaweza kuwa alikuwa anakupenda Ila Matendo yako yakamzingua, Mwanamke ni mwepesi wa kusamehe Ila sio mwepesi wa kusahau, Hii inamaanisha Mwanamke ni kiumbe mwenye Kisasi.
Mwanamke atahitaji Jambo Dogo Sana kuhalalisha chuki yake kwako.
Sisi wajuba, Taikon na Watibeli tunawapa uhuru Wanawake ili wawe na furaha, Mwanamke akiwa na furaha hata wewe utaenjoy mapenzi.
Mwanamke akikupenda na ukamtendea yapaswayo ninakuhakikishia hata Mshahara wake unaweza kuuchukua kama ulivyo.
Ukiona Mwanamke anasema anataka kuhudumiwa au anatanguliza Pesa Mbele tambua kabisa huyo amenyimwa Upendo, hajui kupendwa.
Uhuru na Haki za mwanamke sio kujitenga na wanaume Ila ni kwasababu ya wao kutengwa na Sisi wanaume Jambo ambalo linawafanya wajione sio sehemu ya binadamu au Watu.
Zingatia, usimpe Mwanamke au MTU yeyote mjinga Uhuru. Hataweza kuutumia.
Nawatakie Wanawake wote Happy women's day
Ni Yule Kaka yenu mnayesema anawachukia
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam