Wanawake na ulevi sasa ni aibu kubwa!

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari!

Leo nimekutana na jambo la kushangaza na kusikitisha sana.

Kasumba ya wanawake kuwa walevi kupita kiasi hadi jamii tunaanza kushangaa na kupigwa na butwaa!

Nilikuwa maeneo kama unavyojua siku moja moja hata kama si watumiaji wa alcohol basi huwa tunapenda kukaa mahali na kupata upepo.

Wanawake hawa walikuwa kama gambe basi ilikuwa imefika hadi kwenye unyayo.

Kitu ambacho si cha uungwana kwa hawa viumbe niliokutana nao ni swala la kuona kabisa 'frequency' zimehama baada ya kupiga gambe.

Kama ni kelele basi ni kelele, matusi si matusi, yaani ni vurugu tupu na imani mnafahamu vurugu za walevi wanaume sasa ilikuwa ni wanawake wazuri kabisa.

Ushauri kwa wanawake wenye tabia za ulevi

βœ“ Kama umeamua kupombeka kupita kiasi basi fanya haya chukua gambe ya kutosha weka ndani home piga gambe hali useme basi ila sio kwenye public na kutia aibu hivi.

Nimeshuhudia mambo ya hovyo sana leo na ya aibu kwa hawa walevi ila punguzeni kutumia pombe kupita kiasi.
 
1. Wamejinunulia au waliwezeshwa na sponsa?

2. Wakati wa kwenda kupunguza maji - jojoa walikiwa wanafika maliwatoni au wanaishia njiani..??

3. Walilipa bili yao au walipitisha bakuli kuchangiwa bili?

4. Walicheza mziki kwa midundo ya singeli au rege
 
Namba 4.
Nimeuona mkono wake BWANA Zablon Singers wa Kahama.
 
Nakuaminia Bujii, pale uba utayowakodishia ya kurudi nyumbani itapoishia mlangoni kwako πŸ˜….

Bujii eeehh nipitie basi walau twende tukatoe sadaka J2 leo...
Maana ndo mida hii.
Napokea sadaka zote kwa niaba ya nabii. Fungu la kumi, shukrani ya pekee, sadaka ya Siri nk
 
Napokea sadaka zote kwa niaba ya nabii. Fungu la kumi, shukrani ya pekee, sadaka ya Siri nk


Aahahahahaaaa Bujiiii.....πŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈ

Njoo unipitie bana twende ibada ya pili, tukitoka tunapitia kupata brunch mahala.
 
Aahahahahaaaa Bujiiii.....πŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈ

Njoo unipitie bana twende ibada ya pili, tukitoka tunapitia kupata brunch mahala.
Coming soon, ndio nabeba kitabu Cha nyimbo
 
Ingependeza kama ungetuwekea na picha pia...usikute ni kina Halima Mdee na wenzake au hata majirani zetu.
 

1. Kwa namna yeyote ile kasie matata lazima ustaarabu ushike hatamu.

2. Hapo kwa maliwatoni walijitahidi kufika mkuu.

3. Logically, Kawaida kabisa hakuna uwezekano wa kupitisha bakuli kuchangiwa sehemu kama zile.

4. Hapo kwenye mziki moja niliona mziki wako pendwa ambao ukipigwa sehemu yeyote lazima uinuke.

Swali kwako Kasie Matata, Haya yote yanasadifu nini kwa unywaji ule wa pombe na kelele kwa wanawake wale wazuri?
 

4. Mziki wangu pendwa upi huo??? Naomi’s ntajie maana hapa upako wa kucheza ushanishukia, miguu inawasha... πŸ˜…

Well Pombe ni mada pana sana, kila mmoja anakunywa kwa sababu zake maalum.

Kiujumla tuu hao wadada yawezeakana wamevunja vikoba hapo wanapongezana. Asilimia kubwa wanakuwa ni kikundi kimoja na wanapenda pombe na Mshona was aibu au staha ulishawatoka.
Wengi wao wanakuwa watafutaji hivyo hapo wanajipongeza kutimiza malengo, kodi washalipa, ada washalipa, msosi upo ndani wa mwezi mzima, DSTV, DAWASCO Na LUKU vishalipiwa na hawana mwanaume anayewaendesha.

Ukiachia hayo kuna wale walinyanyaswa sana na wanaume kwenye mahusiano ya mwanzo, sasa wameungana wametiana moyo namna wanaendesha maisha yao bila wanaume.
Hatari ni wale ambao wakitoka hapo kwenye ulevi wanaenda kusagana.

Ila pia Kama ni wanawake wenye watoto, ni vyema wakanywa huko bar na kwenye mahoteli kuliko kunywa nyumbani. Watoto wasione mambo anayofanya mama, wakifanya hayo nyumbani watoto wao wakaona hatari itakuja kwenye malezi na kudhibiti tabia ya mtoto.

Wanawake wanaojielewa wakiwa na hamu wanamalizana na mwanaume hoteli na sio nyumbani kwake.

Alamsiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…