Wanawake na wanaume wenye magari

Wanawake na wanaume wenye magari

Muinjilisti,kwanza naomba ufahamu kuwa lengo la mimi na wewe kubadilishana mawazo kutokana na mitizamo yetu tofauti kwenye hili jambo sio kutafuta mshindi bali ni hoja zitakazopelekea kuisaidia jamii yetu na changamoto zake so sihitaji ushindi!Umesema "unalalama wadada wenye wenye magari huku wakati huohuo wazae kwa uchungu?"Sikia hilo ni tatizo lililotokana na malezi,mtu anataka aolewe au atoke na mwenye gari akifikiri hayo ndo maisha wakati ni kinyume chake!Umesema mifumo imechakachuliwa na ukataja mambo mengi na tabia nyingi mbaya za wanaume kama marioo,kupaka mkorogo nk,kwanza nakubaliana na wewe kua hili ni tatizo but limetokea wapi?Nini chanzo chake?Ukifuatilia utagundua ni tatizo lilelile la malezi,wanaofanya hivyo hawajitambui!Lakini umenishangaza,kwenye mifumo iliyochakachuliwa hukutaja na ule wa mwanamke kuyaacha majukumu yake.Umetaja ujinga wa wanaume tu!Umesema waoaji ni wachache na hao wachache wenye uwezo wa kulea familia ni wachache,pia umesema wengine ni kama akina Eiyer wanataka kuoa halafu hawana kazi!Kwanza tofautisha mtu anaetaka kuoa bila kuwa na plan au malengo na mwenye malengo.Hapa nawazungumzia wenye malengo,yaani unakua kwenye harakati za kuanzisha biashara au unatafuta kazi huku ukitafuta mchumba pia,hapa wakina dada hawawataki hawa,wanawataka wenye magari tayari!Wale wanaotaka kuoa bila malengo wana matatizo na pia ni mada nyingine!
 
Asilimia kubwa ya wanawake wanawaza kuwa na wanaume wenye fedha nyingi, magari mazuri nakadhalika, je ni wanaume wanangapi walivyo navyo hivyo vitu na je, hao wenye navyo wanakidhi idadi ya wanawake wenye uhitaji wa wanaume wenye hivyo vitu. Mwisho wa siku mwanamke kama huyo anahitaji huyo bwana awe wake peke yake huku akiwa kasahau kuwa kampendea mali alizonazo ambapo nyuma yake kuna wanawake wengi wenye kuhitaji bwana mwenye sifa kama za bwana wake.

Mkuu kwa hiyo tusio na magari imekula kwetu!
dah nawaza hapa nijibane vp nami nipate kamkweche kwa kamshahara haka ka vilaki vitatu mbna miujiza kwel kwel.
 
Kwani hao wanavyuo wanasoma milele? Wanaingia mtaani pia. And by the way, hili suala la kubishana, wanawake wengi hapa mjini wanavutika na materialistic things!
kweli kabisa wengi wetu tunapenda material
 
Siku hizi wanaume wenyewe wanahitaji wapendewe pesa zao,
ukimpenda kama alivyo bila fedha anakuona mshamba amini usiamini,
na akipata fedha atakuona haufai na atakwenda mwenyewe kuwatafuta wale watakaompenda kwa fedha.

Wanawake wengi wameumizwa kwa hiyo kilichopo ni kila mtu anaangalia fedha kwanza.
 
Una maanisha atakuwa tayari akuone na mwingine na roho isimuume?

WA Kkuumwa roho wamebakia wacheche sana, wengi ni kuangalia maslahi tu. Watu wanataka pesa kaka. Hata kama wako KUMI, aliye makini atakwambia ni lazima kuvaa NDOMU. Wa ovyo ovyo takwambia kula utakavyo utakapo, kisha cheua hesabu yangu. DUNIA Kushney
 
Wanaangalia maslahi kwanza ndio maana wasichana wengi walio marafiki wanagombana kwa ajili ya mwanaume mmoja ukiangalia vizuri ni mmojawapo katamani mali ya huyo jamaa na then wote wanakuwa vimada... kazi ipo
 
Back
Top Bottom