[emoji1787][emoji1787]Wewe ni mmachame au mmeru?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787]Wewe ni mmachame au mmeru?
Hapa mtafiti akawa ngoswe ,akapotea maboyaSehemu ya PILI
Niliwekwa lockup kwa masaa 48 mpaka yeye mwenyewe alipolia na kuomba waniache kwamba mimi ni mume wake na ananipenda sana hataki niteseke kabisa.NIlishangaa sana alipokuja sero na kuniangalia kwa mahaba na kuniomba msamaha yaishe.Nilipotoka kwa kweli utafiti ulikuwa umekuwa mchungu kwani iligeuka ikawa sasa ni mgogoro wa kimahusiano (Relationship Crisis) Familia yangu kubwa nilikuwa naijali ila upendo kwa mke wangu mkubwa ulikuwa umeshuka sana hasa kwa kuzingatia kwamba niliwekeza akili yangu sana kwa huyu binti wa kimeru.Nilikuwa nimezama kwenye penzi.Sijui kama kuna limbwata au nini ila nilijikuta nakuwa zuzu ghafla.
Maisha yangu yalibadilika,Nalala kwake naamka kwake nashinda ndani tu full time.Maisha yangu yaklivurugika kabisa,biashara zika yumba kipato kikashuka mpaka nikashindwa kulipa hadi kodi.Hali ilikuwa ni tete sana kwangu ili nikiwa naye MOYO wangu unatulia na SHIDA zinaisha akilini.
Kwa sababu mke wangu mkubwa nilimwezesha,alipoona nimenogewa huku aliendelea na maisha yake na mimi nikawa rasmi na binti huyu ambaye sasa alikuwa na miaka 20+Baada ya hali kuwa ngumu sana,Mimi na mrembo wangu tuliama mji tukahamie mji mwingine na kuanza maisha mapya.Wakati hua ameshanizalia katoto kamoja ambako kiuhalisia sikuwa nahitaji kuzaa naye.
Tulianza maisha mapya. ya chini kabisa.Naenda sokoni nanunua mihogo,kongoro,kichwa anapika anauza tunapata riziki.Nilifanya yote haya bila aibu wala hofu kwa sababu nilikuwa naye.Sikuogopa watu kusema huyu msomi anauza mihogo.Sikutaka kuajiriwa bali nilitaka niwe naye tu.
Itaendelea
Wanawake karibia wote huwa na ubinafsi,hii tabia ndo huwa inanifanya niwaogope hawa watu,SEHEMU YA TATU
Pamoja na kwamba tulikuwa tunaishi magumu ila katika familia yangu kubwa maisha yalikuwa kawaida.Kwa sababu mimi nilikuwa navuna nilichopanda sikutaka kabisa wao waathirike kwa namna yoyte ile.Vitega uchumi vyote niliwaachia na huyu binti mpya nilianza naye upya kabisa kujenga maisha mapya kabisa.
Nyuma ya ubongo wangu nilijua kwamba hata kitendo cha yeye kuamua kushika mimba na kuzaa ilikuw ani kuhakikisha kwamba simuachi.Nilimwambia kbisa kwamba nitakuwa na wewe ila hutanimiliko.Neno hili lilimuuma sana kwani najua alitaka kunimilki.Kuna wakati ulifika akaanza kuulizia kuhusu mali zangu nilizokuwa nazo ambazo alikuwa anazifahamu ikiwamo biashara zangu,magari,nyumba na kutaka kufahamu mgao wake na hali yake.Nilimwambia kwamba vile ni mali ya mke mkubwa havimhusu yyey kanipenda mimi basi mimi niko nae aridhike tufanye kazi tutafute mali.
Kauli hii na nyingine nyingi zilimuuma,alikuwa akichukua simu yangu na kumpigia mke mkubwa au kumtumia text na kumwambia aondoke kwenye nyumba yetu aache kungangania pale sio kwake.Alijitambulisha kwa ndugu zangu.Akikuta simu imeandia mama mdogo anapiga simu na kusema yye ni mke wangu anapiga kusalimia.Ndugu zangu walishangaa sana kilichokuwa kinaendelea.
Alikuwa analazimisha nipost picha zake kwenye Social networks zangu na wakti mwingine alichukua simu na kupost mwenyewe ila mimi nilikuwa nazifuta ba kumwambia"Ridhika kwamba Nakupenda na Niko na WEWE.haya mengine ni ziada"
Kwa kweli nilikuwa nampenda ingawa nilikuwa nimeshaona kwamba hanifai.Baada ya Kuona kwamba hanifai nilihitaji kumwacha ila ikawa ni tatizo.Ukizingatia kwamba kulikuwa na mtoto anahusika ilikuwa ni ngumu zaidi.Alikuwa anasema namnyanyasa,nmatesa etc.Niliteseka sana na kukonda sa kwa mawazo kwani nilikuwa katika mtego mbaya sana wa kimahusiano.NILIKUWA NAMPENDA KWA DHATI ILA NILIKUWA SIMTAKI KAMA MKE WANGU"
Kwa kifupi mleta sio mtafiti bali ni mzinzi tu.Hapa mtafiti akawa ngoswe ,akapotea maboya