Wanawake Pemba wakerwa na tabia za madereva Bodaboda kuwashikashika

Wanawake Pemba wakerwa na tabia za madereva Bodaboda kuwashikashika

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Abiria Wanawake Kisiwani Pemba, wamelalamikia tabia ya baadhi ya madereva wa pikipiki ‘boda boda’ kuwaingia mwilini wakati wanapokuwepo kwenye vituo vyao, kutaka usafiri wa aina hiyo.

Walisema mara unapofika kwenye eneo lao la vituo na kutaka usafiri, huvamiwa na kuanza kukukopea mizigo na wengine kuwashika mikono, wakivutiana kwenye chombo chake.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye eneo la Mtuhaliwa wilaya ya Mkoani Pemba, walisema wamekuwa wakisikitishwa na tabia hiyo.

Mmoja kati ya wanawake hao aliyekataa jina lake lichapishwe alisema, baadhi ya waendesha boda boda hao, wamekua wakiwaingia mwilikini, kwa lengo la kufanya ushawishi.

Alieleza kuwa, kinachowaudhi ni kule kuanza kupokea kuanzia mizigo mikubwa hadi vipochi vya mkononi, na wengine kukumata mikono.

‘’Ukiteremka gari tu, wanaaza kukuzonga, wengine wanakupokea hata vipochi vyenye simu, na wengine wanaanza kukushika shika mikono, wakitaka upande boda bado yake,’’alisema.

Kazija Issa Mohamed wa Mwambe alisema, juzi kwenye kituo cha boda boda cha Mtambile-Kengeja aliangushwa chini, baada ya waendesha boda boda, kuvutia mkoba wake.

Alieleza kuwa, mara alipoteremka gari akitokea Chake chake, alishuhudia ameshadakwa na wendesha boda boda, na kuvutwa kwa ghafla mkoba wake na kuanguka chini.

‘’Hawa waendesha boda boda baadhi yao sio wastaarabu, maana wamekuwa wakituingia maungoni kutaka abiria, jambo ambalo sio zuri,” alieleza.

Kwa upande wake Mmanga Haji Kassim, alisema juzi mume wake aligombana na mwendesha bodaboda eneo la Kenya-Chambani, baada ya kumvamia mke wake.

“Ni kweli waendesha bodaboda wengi wao hawana nidhamu, maana mimi juzi kushuka gari wakati mume wangu yupo na usafiri ananisubiri, yeye ameshanikamata mkono,’’alilalamika.

Mwendesha bodaboda wa njia ya Mtambile-Kengeja Mohamed Haji, alisema wamekuwa wakikatazana jambo hilo, ingawa badhi yao wapo watukutu.

“Ndio maana tulitaka tuweka zamu, ili kuepusha hilo, lakini bado hatujakubaliana na ndio maana, tumekuwa tukishtumiwa kuwafanyia vurugu abiria hasa wa kike,’’alieleza.

Mwendesha bodaboda wa Machomane Chake Chake, Issa Kassim Issa, alisema nidhamu na ustaarabu ndio jambo ambalo wamekuwa wakisisitiza kila siku na viongozi.

Mwenyekiti wa waendesha bodaboda mkoa wa kusini Pemba Kassim Juma, aliwataka abiria wanawake kuripoti katika vyombo vya sheria, wanapogundua kuvunjiwa haki zao.

‘’Hakuna hata bodaboda mmoja, aliyeruhusiwa kumvamia abiria, bali kama kuna zamu ndio jambo jema kama hakuna, aulizwe kistaarabu,’’alisisitiza.

Hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mattar Zahor Massoud aliwataka waendesha boda boda hao, kutojihusisha na kitendo cha aina yoyote, kinachoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.

Kwa sasa kisiwa cha Pemba kina wastani wa bodaboda 300, zikiwemo zile zilizotolewa kwa njia ya mkopo kutoka kwa Rais wa Zanzibar chini ya benki ya CRDB na wafadhali wengine.

Chanzo: pembatoday
 
Hawapendi tokea zamani, au baada mfungo kuanza?

Mwanaume hawezi from nowhere kumshika mwanamke sehemu za mwili wake intentionally, bila kuwa ameoneshwa indications zotote. Labde awe sio timamu kichwani
 
Hao wanawake nao waache uchoyo wao.
Kushikwa tu kuna ubaya gani?

Ingekuwa wameingizwa nyama bila mfupa kweli ingekuwa noma.
Sitaki povu hapa.
 
Hawapendi tokea zamani, au baada mfungo kuanza?

Mwanaume hawezi from nowhere kumshika mwanamke sehemu za mwili wake intentionally, bila kuwa ameoneshwa indications zotote. Labde awe sio timamu kichwani
Huwajui boda boda na wapiga debe stands.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Abiria Wanawake Kisiwani Pemba, wamelalamikia tabia ya baadhi ya madereva wa pikipiki ‘boda boda’ kuwaingia mwilini wakati wanapokuwepo kwenye vituo vyao, kutaka usafiri wa aina hiyo...

Hili nalo mkaliangalie
 
Hawapendi tokea zamani, au baada mfungo kuanza?

Mwanaume hawezi from nowhere kumshika mwanamke sehemu za mwili wake intentionally, bila kuwa ameoneshwa indications zotote. Labde awe sio timamu kichwani
Umesoma ukaelewa au unaleta ujuaji usio na tija. Bodaboda ni kazi ya laana mara nyingi ukishuka tu kwenye basi wanakuzonga. Juzi kuna dada mmoja kavunjwa mguu. Hawa utaratibu wa kazi yao. Tumia vizuri kichwa chako sio kubebea funza.
 
Tatizo lililopo ni hao wanawake kushindwa kuonyesha kuchukizwa na hiyo tabia tangia mwanzo na ndio sababu imeota mizizi.

Kwani kikawaida bodaboda huwa ni watu wenye tabia ya kujaribu jaribu.
 
Mmoja kati ya wanawake hao aliyekataa jina lake lichapishwe alisema, baadhi ya waendesha boda boda hao, wamekua wakiwaingia mwilikini, kwa lengo la kufanya ushawishi.
Chanzo: pembatoday
Katika bandiko la jamaa, point yangu iliegemea hapa. Na bado nasisitiza, hakuna mwanaume anayeza kumuingia mwanamke maungoni, bila kuwepo na viashiria alivyopewa.

Umesoma ukaelewa au unaleta ujuaji usio na tija. Bodaboda ni kazi ya laana mara nyingi ukishuka tu kwenye basi wanakuzonga. Juzi kuna dada mmoja kavunjwa mguu. Hawa utaratibu wa kazi yao. Tumia vizuri kichwa chako sio kubebea funza.
Kuna watu huwa nawashangaa sana, huwa hamuwezi kutetea points zenu kwa hoja au staa ili mueleweke, lazima mtukane. Kwa haraka haraka, sidhani kama una matumizi mazuri na kichwa chako mkuu. No offense
 
Huwajui boda boda na wapiga debe stands.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nawajua vizuri sana na fujo zao. Ila ninachokataa, ni kusema huwa wanawaingia maungoni kwa lengo la kufanya ushawishi.

Hivi mtu anayehitaji kukuhudumia ili apate hela yako, anaanzaje kukushika sehem mbaya??? Unless muwe na mazoea ambayo mmeyajenga
 
Hapo sawaaa nimekuelewaa.
 
Nawajua vizuri sana na fujo zao. Ila ninachokataa, ni kusema huwa wanawaingia maungoni kwa lengo la kufanya ushawishi.

Hivi mtu anayehitaji kukuhudumia ili apate hela yako, anaanzaje kukushika sehem mbaya??? Unless muwe na mazoea ambayo mmeyajenga
Hata kumshika mkono kwa mwanamke ni sehem mbaya, kumbuka hao wanaolalamika ni wanawake wa kiislam
 
Back
Top Bottom