Niliwahi kuandika humu kusiana na rafiki yangu mmoja ambaye ni mtendaji wa mlandege & mumewe alikuwa mwalim wa tagamenda sekondari.kwa kweli rafiki yangu alikuwa anamnyanyasa sana mmewe na kila alie mshauri alimjengea chuki.
Rafiki yangu huyu hakutosheka kumuweka mumewe ndani tu mara kadhaa alidiriki hata kumnyima chakula. Huyu baba alivumilia yote hayo kwa kuwa wamezaa watoto wawili na wamefankiwa kujenga huku kitwiru Iringa. Baba huyu ni mlokole na kwakweli hajui kubishana kabisa yaani unaweza ukahisi labda anashida.
Sasa shosti ameenda mahakamani kaomba talaka na anataka nyumba iuzwe kila mtu apewe chake .Baba wa watu hataki nyumba iuzwe wapewe watoto lakini mwanamke hataki. Nyumba yao ni nzuri tu. Sasa shosti anashinda manispaa akiwashawishi wathaamini WAISHUSHE nyumba gharama ili amkomoe aliekuwa mme wake.
Mahakam iliamuru mme apewe 40 %na mke 60. Sasa baba wa watu ametaa kuhama kwenye nyumba mpaka atakapojua hatma ya nyumba yao.
SASA SHOSTI YUKO ANASUKA MPANGO WA KUMBAMBIKIA KESI YA UBAKAJI KUPITIA KWA BINTI WA KAZI.
Kuna binti amemchkua kwa rafiki yake kwa kazi hiyo. Na kuna mwanaume anasuka mpango huo anaitwa Stivu.
Bahati mbaya likizo huyu baba ameenda kwao lakini akirudi huu ndo mkakati uliosukwa.
MUNGU TUSAIDIE NA UTUSAMEHE DHAMBI ZETU. MOYO WANGU UNAAMANI KWA KUUFICHUA UKWELI HUU.