SoC02 Wanawake tuinuke, huu ni wakati wetu

SoC02 Wanawake tuinuke, huu ni wakati wetu

Stories of Change - 2022 Competition

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra kusikia mijadala inayohusu uwezo wa mwanamke katika kuongoza, ilionekana mwanaume ndiye anafaa.

Dhana hii inazidi kukosa mashiko kadiri siku zinavyokwenda kutokana na ufanisi unaoonekana kwenye nafasi zilizoshikwa na wanawake. Wanawake wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wengine kuwania uongozi.

Rais Samia Suluhu ni miongoni mwa viongozi wanaowavutuia wananwake wengi katika utendaji kazi na kuwashawishi wengine wawanie uongozi wakipata fursa za kufanya hivyo.

Hivi sasa nafasi kubwa za uongozi nchini zinashikiliwa na wanawake na wanafanya kazi nzuri inayoonekana na hivyo kuzidi kuhamasisha wanawake wengine kujiamini na kuchangamkia nafasi za uongozi kwani kila kitu kinawezekana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom