Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Licha ya kuwa mshikakijiti ni mwanamke mwenzao, bado ngome ya wanawake CCM haina kifua cha kuwafanya watembee kifua mbele dhidi ya mfumo dume wa chama chao. Haya sio maneno yangu, bali ni uhalisia uliopo kwenye orodha ya wagombea wa awali wa CCM kwa nafasi za ubunge na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Huwezi kuamini kwamba wamekosa hamasa hadi wamekuwa 21.6% tu ya wagombea 1,199 katika mikoa 29, hii ni wazi chama kinashindwa kufikia lengo la kitaifa la 30% la uwakilishi wa wanawake bungeni, na kimeshindwa kimfumo kutoa kipaumbele cha usawa wa kijinsia bila ya msaada wa viti maalum.
Mikoa mingine ndio imetiahaibu kabisa. Mara (7.5% ), Rukwa (7.1%), na Simiyu (9.3%) yaani ni timu za kiume pekee, huku maeneo kama Bunda na Sumbawanga Mjini hayana hata mwanamke mmoja. Hata katika maeneo yenye uwakilishi bora kama Kusini Pemba (41.2%) na Mjini Magharibi (34.7%), wastani wa kitaifa unaonyesha wazi: Ngome ya wanawake ya CCM bado haina uthubutu vya kutosha wa kutwaa nafasi za kiushindani. Maeneo kama Uyole (100% wanawake) hayawezi kubadili uhalisia kuwa bado wanawake wa CCM hawana Kifua cha kuwafanya watembee kifuambele.
Hili sio suala la idadi tu, ni suala la ujasiri wa ngome hiyo au chama kuwaamini wanawake kwenda kwenye nafasi za kiushindani. Orodha inaonyesha wazi chama kimebweteka kwenye kutegemea viti vya maluum kufikia malengo ya usawa wa kijinsia na kujenga ngome ya wanawake wenye ujasiri wa kushindana na wanaume waliotawala kwenye chama hicho.
Kushindwa kwa CCM kuteua wanawake wengi zaidi katika mikoa kama Njombe (10.3%) au Iringa (10.8%) kunaashiria ukosefu wa nia ya kisiasa ya kuvunja miiko ya dhana kuwa chama hiko kinatawaliwa na wanaume. Kama ngome ya wanawake inataka kuthibitisha uwezo wake wa wanangome yao, lazima idai zaidi ya uwakilishi wa kiushindani, lazima iwe na wagombea wanaoweza kusimama kidete na kushindana moja kwa moja na hali iliyopo. Orodha haidanganyi, Wanawake wa CCM bado hawana kifua cha kutembea kifuambele.