Wanawake wa Dar na Njombe waongoza kwa kujifungua kwa njia ya upasuaji. Shida ni nini?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Hivi kwanini siku hizi wanawake wengi wanapenda kujifungua kwa oparesheni? Au ni fashion wakuu?

=====================================

Wajawazito wanaoishi katika mikoa ya Njombe, Dar es Salaam na Iringa wametajwa kuvuka kiwango cha idadi ya kujifungua kwa njia ya upasuaji, hali inayoashiria baadhi yao wanafanyiwa bila sababu za msingi za kitabibu.

Mkoa wa Njombe umetajwa kuongoza kwa kuwa na asilimia 32 ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji, Dar es Salaam asilimia 26 na Mkoa wa Iringa ni asilimia 24.

Hali hiyo imetajwa kuwa ni kinyume na mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) linalopendekeza wastani wa wanaojifungua kwa upasuaji uwe chini ya asilimia 12 mpaka 15 kwa eneo husika.

Hayo yameelezwa jana jijini Arusha na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dk Hamad Nyembea wakati akitoa mada kuhusu hali ya utoaji huduma za afya nchini, kwenye kongamano la kitaifa la tiba linalokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

Amesema hali hiyo inaashiria wajawazito wengi wanafanya uamuzi wa kufanyiwa upasuaji bila ulazima wowote na kwamba hiyo ni miongoni mwa changamoto za kitaalamu zilizopo katika huduma za uzazi, na huenda inatokea wananchi wakiwa hawana uelewa.

"WHO inapendekeza wastani wa wanaojifungua kwa upasuaji uwe chini ya asilimia 12 mpaka 15, lakini kuna baadhi ya mikoa imefanya upasuaji wa kina mama zaidi ya kiwango hicho, hii inaashiria huduma za upasuaji zinafanyika pasipo na sababu za msingi," amesema.

Source: Mwananchi
 
watu wa dar wengi wanatatizo la lishe duni, wanakula ila vyakula vibovu, wanawake wao wamezidi hata kula vizuri hawali.
Pia siku hizo mjni kumeingia fashion ya kuzaa kwa upasuaji ili kutunza uchi uwe katika hali nzuri.

Kwa njombe sielewei kitu.
 
Hivi kwanini siku hizi wanawake wengi wanapenda kujifungua kwa oparesheni? Au ni fashion wakuu?

=====================================

Wajawazito wanaoishi katika mikoa ya Njombe, Dar es Salaam na Iringa wametajwa kuvuka kiwango cha idadi ya kujifungua kwa njia ya upasuaji, hali inayoashiria baadhi yao wanafanyiwa bila sababu za msingi za kitabibu.

Mkoa wa Njombe umetajwa kuongoza kwa kuwa na asilimia 32 ya wanawake wanaojifungua kwa upasuaji, Dar es Salaam asilimia 26 na Mkoa wa Iringa ni asilimia 24.

Hali hiyo imetajwa kuwa ni kinyume na mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) linalopendekeza wastani wa wanaojifungua kwa upasuaji uwe chini ya asilimia 12 mpaka 15 kwa eneo husika.

Hayo yameelezwa jana jijini Arusha na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dk Hamad Nyembea wakati akitoa mada kuhusu hali ya utoaji huduma za afya nchini, kwenye kongamano la kitaifa la tiba linalokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

Amesema hali hiyo inaashiria wajawazito wengi wanafanya uamuzi wa kufanyiwa upasuaji bila ulazima wowote na kwamba hiyo ni miongoni mwa changamoto za kitaalamu zilizopo katika huduma za uzazi, na huenda inatokea wananchi wakiwa hawana uelewa.

"WHO inapendekeza wastani wa wanaojifungua kwa upasuaji uwe chini ya asilimia 12 mpaka 15, lakini kuna baadhi ya mikoa imefanya upasuaji wa kina mama zaidi ya kiwango hicho, hii inaashiria huduma za upasuaji zinafanyika pasipo na sababu za msingi," amesema.

Source: Mwananchi
kwa wanawake wa dar nadhani inawezekana ni mambo ya pwani yameharibu kila kitu wanaona aibu kwenda kutoa hewa upande wa pili wakati wa kujifungua. ila kwa wale wa njombe, ni kimo, ni wafupi. majority ya wanawake wafupi huzaa kwa operation hasa wakizaa na mwanaume mrefu.
 
Back
Top Bottom