Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wanawake wa Jamii ya wahadzabe wanaoishi katika eneo la Eyasi wilayani Karatu Mkoani Arusha wamepaza sauti katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kumuomba Rais Samia Suluhu awasaidie wapate ardhi,maji,chakula na kuzuia uvamizi wa maeneo yao.
Katika mdahalo uliofanyika katika Kijiji cha Qandet eneo la Eyasi Wilaya ya Karatu, na kuandaliwa na taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) kwa kushirikiana na Kituo cha Radio cha SAVVY FM, ambao wametoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake na watoto.
Katibu wa Wahadzabe eneo la Eyasi, Maria Yona amesema“tunatamani sana kumuona Rais Samia Mwanamke mwenzetu, tumweleze sisi wanawake wa Kihadzabe tunavyoishi katika maisha magumu sana, hatuna maji, hatuna ardhi na chakula”anasema.