Wanawake wa Mbeya wanajua sana kulia msibani

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Nimehudhuria misiba kibao ila msiba ukutane na wamama wa Mbeya. Aisee! Unaweza hata kulia na wewe, wanajua sana kuangusha kilio. Utakuta mama ametoka alikotoka anafika karibu na palipo msiba, umbali wa kama mita 30 hivi basi anapiga bomba moja la yowe mji mzima unaamka kwa kilio halafu baada ya dakika 5 tu wakavu hawana hata tone la chozi.

Sasa sijui ni utamaduni wao au wanaguswa sana na misiba?
 
Mila kaka! Mimi niliona Buja watu hawalii wanakuja wanasalimia wanaanza kupiga mtungi yaan anayekuja msiban kama ana uwezo kidogo basi hatokosa kuja japo na kreti mbili watu wanakula kidang'a kwanza alafu sasa kama utataka kuangusha kilio ndio na wenzako wanakipokea sasa mko bwax.
 
Kama wamama wa kijaluo, wanakuja msibani wako poa kabisa story kibao njiani. Wakikarlibia msibani wanakubaliana nani alianzishe, akianza mmoja kincchofuata ni kilio cha mwaka ukiwa mgeni utabaki na butwaa. Baada ya muda wakifika wananyamaza, stori zinaendelea na misosi ya kufa mtu plus muziki wa nguvu na pombe.
 
Ha ha ha ha yaani halafu ni lazima ulie huku unaongea, mimi ni mnyakyusa ila hii mila imenishinda.

Nilienda kwenye msiba hata siwajui njiani tukaambiwa tukifika karibu tuanze yowe.

Yani kila nikitaka kulia machozi hayaji niliabika siku ile maana watu wanakuja wanatupokea mimi natoa tu macho.
 
i
eti wanakubaliana nani alianzishe😂😂😂😂
Yaani kweli kabisa mkuu, kitambo msiba unakaa hata wiki 2 hadi 4 wanasubiri ndugu wote wa marehemu wafike. Muda wote huo ni pombe, msosi na muziki. Wakisikia wageni wameanzisha kilio huko nje wanapokelewa kwa kilio na wenyeji ghafla wanamute na stori zinaendelea. Umenikumbusha mbali mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…