Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Nimehudhuria misiba kibao ila msiba ukutane na wamama wa Mbeya. Aisee! Unaweza hata kulia na wewe, wanajua sana kuangusha kilio. Utakuta mama ametoka alikotoka anafika karibu na palipo msiba, umbali wa kama mita 30 hivi basi anapiga bomba moja la yowe mji mzima unaamka kwa kilio halafu baada ya dakika 5 tu wakavu hawana hata tone la chozi.
Sasa sijui ni utamaduni wao au wanaguswa sana na misiba?
Sasa sijui ni utamaduni wao au wanaguswa sana na misiba?