Wanawake wa Mpanda walia na waume zao kukimbia majuku ya familia

Wanawake wa Mpanda walia na waume zao kukimbia majuku ya familia

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wababa wa Mpanda mbona hivyo lakini?

Ila wanaume wengi wa mikoani wamekuwa wategevu kwa namna fulani katika kujishughulisha na majukumu ya kuelea familia, hii sasa ni balaa na tabu tupu!
==================
Kampeni ya msaada wa kisheria ya "Mama Samia Legal Aid Campaign" inaendelea mkoani Katavi, ikilenga kutoa elimu na usaidizi wa kisheria kwa wananchi. Wanawake wa Kata ya Kanoge, Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, wameeleza changamoto zinazowakabili, wakilalamikia tabia ya waume zao kulala mpaka saa sita mchana pasipo kujishughulisha na kazi za uzalishaji wala kutoa msaada kwa familia.

Bi. Paulina Marco, akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, ameeleza kuwa wengi wao wanalazimika kuchakarika kwa kazi za shambani na majukumu ya nyumbani wakiwa na watoto wao, huku waume zao wakikwepa jukumu la kuhudumia familia. Pia ametaja kuwa baadhi ya wanaume wanakunywa pombe kupitiliza, hali inayochochea vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo vipigo, ambavyo vinaathiri watoto kisaikolojia.

 
Back
Top Bottom