Siko hapa kuwakebehi wanawake ama dada zetu lakini hii habari ni ya ukweli na iko-based na my own personal experience huko ughaibuni na kwa sasa hapa Dar. Nimejaribu mara kadhaa kutafuta rafiki kwaajili ya dating then kama chemistry ipo na tuna-click basi sitosita kuendelea kumpenda ambaye tutapatana ili eventually tufunge ndoa na nitulizane na mwenza wangu ili tuendelea na safari ya maisha.

Baada ya kuwasaka akina dada wa mitaani/makazini/makanisani na miskitini etc. bila mafanikio nikaona sasa nihamie online dating, ambako nimekutana na wanawake wa aina mbalimbali lakini tatizo wanawake wengi wa mtandaoni sio wakweli.

Utakuta mtu kaweka kwenye profile picha yake nzuri anapendeza na anavutia. Lakini tukikubaliana tuonane nakuwa nabaki mdomo wazi.

1. Unakuta kwanza hiyo picha kumbe ni ya zamani alipokuwa bado umri haujaenda na akitokea unakuta umri umekwenda

2. Mdada ni mnene zaidi transforma wakati alisema kwenye profile yake kuwa maumbile yake ni slim/average.

3. Anadai ktk profile yake kuwa ni mrefu kumbe ni mfupi. n.k.

Nimeshakutana na wadada 13 (8 ughaibuni 7 hapa hapa Dar) na mara zote nimepoteza muda wangu na pesa zangu kwaajili ya hizi dates na kuambulia kulipia gharama za dinner, wine, taxi etc at expensive restaurants.

Swali:

1.Je wanawake wanaotafuta wapenzi online ni wale ambao hawavutii kimaumbile na wako desperate?

2. Kwa nini akina dada hawako wakweli ktk online profiles zao? mnaweka picha za zamani, mnadai wembamba kumbe wanene?