Wanawake wa siku hizi wachapa kazi

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Niwape pongezi kubwa wanawake wamejitoa kwenye utegemezi na wanachapa kazi kweli kweli. Kule kuchagua kazi kumeisha na sasa hivi utawakuta maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye udereva, kondakta, hata wamachinga wanaouza vitu kwenye daladala. Kazi ambazo hapo awali iliaminika ni za wanaume.

Nimepita maeneo ya mbezi mwisho pale stand nikaona asilimia kubwa ya wachuuzi wa vitu kama maj, biskuit, karanga, pipi nk ni wanawake!

Hapo zamani ilizoeleka ni kazi za wanaume tu
Hongereni wanawake kwa mwamko
 
Mji umekuwa mgumu usipofanya kazi hauli
 
Njombe ni kawaida kabisa hiyo tangu enzi na enzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…