"Wanawake wa siku hizi wanadeka sana"

sasa mjini hapa wakalime lami? Mashamba hakuna nyumba ya kupanga sinza cjui manzese. Hebu waacheni wajawazito wa watu

Kazi sio kulima tu mkuu!
Kauli yako inafanana sana na ya yule aliyesema: "Tatizo la umeme linatokana na ukame, na serikali haina uwezo wa kutengeneza mvua".
 

Mgongano wa mawazo!
 

Sio kwa sababu ya mtandao huu?


 
Nakubaliana kabisa na mkeshaji kuwa wadada siku hizi tuna uvivu. Ndio maana kasi ya caesarean imekuwa kubwa tena wengine wana uwezo kabisa wa kudeliver normal lakini hawataki. Ila kingine pia najaribu kufanya utafiti lakini kwa wale wenzetu wanaotumia njia ile ambayo si halali ufanya tendo la ndoa hawawezi kudeliver normal. nadhani mkeshaji tusaidiane na hili.
 

He! we Laura! Tusaidiane vipi tena hapo jamani.
 
Yaani nimecheka hadi my baby in my stomach ameruka kwa furaha. Sina uhakika sana na hicho mnachokisema maana hapa nilipo nipo kazini napiga kazi kwa kwenda mbele, na ukiona siji ofisini ujue am about to give birth. Hata hivyo kwani kudeka mnakokuzungumzia ni kupi? naona mnachanya mada hapa, kuna kudeka na uvivu hivyo ni vitu viwili tofauti, kudeka kwa nani nayo ni issue nyingine, kama mwanamke ana deka kwa mume wake hilo ni tatizo jamani! ebu tuwe wakweli, kudeka ni sehemu ya mapenzi au nyie hamjui?, yes it is
 

Kuna aina ya kudeka bana Aine sio ushindwe kufua vikufuli vyako vikatakata then umpe kazi hiyo kazi hiyo housegirl then utuambie eti unadeka!
 
Kuna aina ya kudeka bana Aine sio ushindwe kufua vikufuli vyako vikatakata then umpe kazi hiyo kazi hiyo housegirl then utuambie eti unadeka!
Kudeka si kumpa house girl kazi asiyostahili, unadeka mkiwa na mume wako tena chumbani na si sebuleni mbele ya watoto, kushindwa kufanya kazi kwa mwanamke mjamzito ni uvivu na hulka ya mtu binafsi hata asipokuwa mjamzito labda ashindwe kufanya kazi kutokana na complications mbalimbali, mfano anaweza kuwa recommended na daktari asifanye kazi lakini ktk hali ya kawaida kuna baadhi ya kazi anazifanya kama kawaida tu
 
na wanaona kudeka ni haki yao bila kupima effect zake. tena ni wagumu kupokea ushauri, matokeo yake operation. eti kwenda na wakati. kudeka km wahindi veve lisha mimi!
 

Mimi sikubalini na huyo Gynacologist kuwa sababu ya Caesarean sections nyingi siku hizi ni 'kudeka' kwa wanawake! Kwa kiasi kikubwa naamini haya ni matokeo ya maendeleo katika 'emergency obstetric and newborn care (EmONC)' katika kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga. Hospitali na vituo vingi vya afya vimewezeshwa kuweza kufanya Caesarean section kwa wamama ambao progress yao ya labor si nzuri au wale wenye viashirio vya kushindwa kujifungua kawaida.

Miaka ya nyuma, hata miaka ya mwanzoni mwa 2000s huduma ya dharura kwa mama wajawazito ilikuwa mbaya na haipatikani, lakini sio kwamba kulikuwa na akina mama wasiohitaji upasuaji! Wengi wa waliohitaji hawakupata wakashia kufa na walisurvive wengi kupata matatizo mbali mbali including fistula. sasa hivi hali ni afadhali, na wengi wao wanapata huduma hiyo...hivyo kwa sababu wanaopata ni wengi inaonekana 'mideko'...sikubali!
 

hapo nimekuele then hata huko chumbani hutakiwi kudeka mpaka iwe kero! Mana ktk game unaweza ukaambiwa kaa hv unaana ooh naumia,mara ooh sijisikii.
Mjue mikiki mikiki ya game ni mazoezi tosha hadi mtoto anachamka tumboni.
 
Mwaka kesho nitadeka saaaaaaana yani hadi kuogeshwa
 
Wanaodeka ni wanawake wanaoishi mijini. Huko kijijini, we acha tu mambo Mama anjifungua akiwa anachunga ng'ombe, baada ya hapo anabeba mtoto na kuswaga ng'ombe kuwarudisha nyumbani. Enyi Wamama wa Bongo, A'town, Rock city n.k endelea kudeka tu lakini mkifahamu kuwa hali ni tofauti kwa wenzenu walioko vijijini.
 
Kuna jirani yangu mkewe ka-deliver jana kwa ceaserean section.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…