Wanawake; wafanyeni wanaume zenu wanukie vizuri

Wanawake; wafanyeni wanaume zenu wanukie vizuri

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Siku moja nilikuwa nimeuzuri kikao cha kiutendaji na wanachama wa taasisi A.

Karibu yangu nilikuwa nimekaa na mbaba mmoja, ana kama miaka 45 hivi. Ni mtu mwenye nafasi nzuri tu, na kipato si kibaya, kwa sababu anaweza kuwa na 'net' ya m. 5 kwa mwezi; achilia mbali mambo mengine.

Kilichonisikitisha; ni mwili, mdomo kutoa harufu ambayo si rafiki kwa watu waliokaa naye karibu. Kwangu nilitamani muda ukimbie ili kikao kiishe haraka, tuweze kuondoka.

Nikajiuliza, mkewe ameshindwaje kumbadilisha mumewe ili awe ananukia vizuri?

Kwa sababu sisi wengine, wake zetu ndio wanatupangilia mavazi ya kuvaa, sabuni nzuri za kutumia, mafuta na manukato mazuri ya kutumia.

Mi nadhani, lawama zote ziende kwa mkewe.​
 
[emoji16] Aisee mimi kaka mimi kunuka mdomo hapana hata nigonge wiki bila kuswaki sinuki
 
Wake wengine kila jioni ni lazima uoge hata kama ni baridi kali, usipooga hupewi shoo, pia ni lazima ubadilishiwe boxer kila unapotoka bafuni kuoga. Wanawake hao wako vizuri kuhakisha waume zao ni wasafi kila wawapo
 
Siku moja nilikuwa nimeuzuri kikao cha kiutendaji na wanachama wa taasisi A.

Karibu yangu nilikuwa nimekaa na mbaba mmoja, ana kama miaka 45 hivi. Ni mtu mwenye nafasi nzuri tu, na kipato si kibaya, kwa sababu anaweza kuwa na 'net' ya m. 5 kwa mwezi; achilia mbali mambo mengine.

Kilichonisikitisha; ni mwili, mdomo kutoa harufu ambayo si rafiki kwa watu waliokaa naye karibu. Kwangu nilitamani muda ukimbie ili kikao kiishe haraka, tuweze kuondoka.

Nikajiuliza, mkewe ameshindwaje kumbadilisha mumewe ili awe ananukia vizuri?

Kwa sababu sisi wengine, wake zetu ndio wanatupangilia mavazi ya kuvaa, sabuni nzuri za kutumia, mafuta na manukato mazuri ya kutumia.

Mi nadhani, lawama zote ziende kwa mkewe.​
Wanaume wengine wabishi jamani[emoji119]
Aah!
 
Jmn wengine tunapenda mwanaume anaenukia .ila Kuna wanaume wabishi

Hasa mtu hata kuswaki issue hiyo [emoji182] inakuaje ss
 
Ntakupa mfano sijajua wengine nilikaa na wadigo wako ivi ikitokea mwanamke mumuwe ana matatizo labda kunuka ,kutokuvaa vizuri basi moja kwa moja analaumiwa mkewe na kuchekwa 😅😅😅

Sasa sijajua jamii nyingine ni ngumu sana kukuta aliyeoa mdigo ananuka kama mbuzi ila wanakera kuna jamaa anakuja job enzi izo nipo intership taasisi fulani ananukia maperfyume ya kiarabu watu pale wanamsema jamaa ananukia aliingia tu utajua na nguo ndo usiseme kila shati jipy analo
 
Happ Lina kitambi harufu inatoka tumboni sasa akirudi kunywa supu tuwe wasafi wanaume mbona watu wasafi kibao mtu una hela ila unanuka kama mbuzi
 
Unuke kinywa lawama apewe mwanamke, unuke kwapa lawama apewe mwanamke, naimani 85% ya wanawake wote duniani hupenda mume wake au mpenzi awe msafi lakini akikutana na kimeo ndio inambidi avumilie tu mlee watoto, na ukiona uchafu kwa mwanaume umezidi tambua hata mke wake ni mchafu, kwa mfano unalala vipi usiku bila kusafisha kinywa wala kuoga
 
Back
Top Bottom