Wanawake wajawazito wanajifungulia sakafuni Hospitali ya Buzurugwa

nuporo

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2018
Posts
1,534
Reaction score
3,387
Nimeona comment nyingi wanawake wanasema wanaporwa simu wanapoenda labor huko hospitali za serikali. Wanawapora simu sababu hii, hawataki watanzania waone kuwa in 2023 bado wanawake wanazalia sakafuni.. Hii ni hospitali ya Buzurugwa.

Wamama wanapeana zamu kuzaa sakafuni. Na hii ndo situation hospitali za serikali na wanaficha kwa kuwanyang’anya simu wamama ila kuna mama mmoja alienda na simu mbili wakachukua moja kumbe ingine kaificha ndo akachukua matukio. Huyu mama alikuwa kapata experience mbaya before so this time around akataka kuchukua ushahidi.

CCM Tanzania muogopeni Mungu in 2023 kweli bado wanawake wanazalia sakafuni? Hizo tozo mnapeleka wapi?
 
Jiji la Mwanza wamefikia wapi kuhusu ujenzi wa Hospital ya Jiji?

Mwisho nyie mnaopiga picha wamama Wakiwa uchi mnatakiwa kushtakiwa Kwa kuharibu privacy Yao
 
Kama sehemu ambayo inabidi ipewe kipaumbele basi ni kuboresha huduma ya wamama wajawazito , serikali ilitazame kwa ukaribu .
 
Sasa mnapiga picha wamama wa watu wakiwa uchi ,hivi mna Akili kweli?
Angekua mama yako ungefurahi?
Nyie watu mna matatizo ya akili
 
Nimeogopa. Namshukuru Mungu kwa maisha yangu kwakweli sijawahi pitia huko. Hali kama hiyo huyo aliyewekwa kitandani ukute ameshatoa chochote kitu. Hosptali za serikali zinakatisha tamaa kuzikaribia
 
Aisee nategemea Mama aweke hili liwe kipaumbele chake anajua maumivu ya kina Mama..
 
Nimeogopa. Namshukuru Mungu kwa maisha yangu kwakweli sijawahi pitia huko. Hali kama hiyo huyo aliyewekwa kitandani ukute ameshatoa chochote kitu. Hosptali za serikali zinakatisha tamaa kuzikaribia
Hajatoa chochote nakuhakikishia
Hali ipo hivyo kwenye vituo vya afya, Labor kuna kitanda kimoja ,wamama wanaojifungua wapo watatu, mwingine anakuja tayari uchungu ushakolea,mtoto ashatoa kichwa wakati huo kitandani kuna mama nae anajifungua, utafanyaje kwenye Hali kama hiyo Zaidi ya kumuweka chini
Ukweli Ni kwamba huduma za afya bado Ni changamoto kweli kweli, watumishi wachache,miundombinu mibovu, ila watu wanachoangalia Ni kuwaangushia lawama watumishi huku wakiacha serikali.
 
Lawama ni kwa serikali maana mtumishi hana kosa lolote hapo. Yeye anachojitahidi ni mama na mtoto wawe salama, mazingira gani ndio mpambane na hali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…