Nahisi tunashindwa kuelewa kuwa zamani watu walioana kwa kuchaguliwa na wazazi, mtu alikuwa haowi au kuolewa bila wazazi wake kuridhia kuwa mwoaj/mwolewaji ndiye kweli chaguo lao, so issue za kutongozana hata kama binti angekubali sidhani kama ilikuwa ikijulikana kwani kwa kufanya hivyo kungeweza kumzibia riziki ya kuolewa.
Sasa kwa wakti tulio nao wazazi hawana nafasi tena ya kuwapangia vijana machaguo yao, hivyo kila upande hasa (kwa wasichana), kwa sababu ni free market inabidi wasiringe saana kama ilivyokuwa hapo awali. Na wanaume nao siku hizi si waoaji, unakuta mtu ana machaguo hata matano, kwamba akikataa huyu najaribu kwa huyu, kwa sababu sasa ni dunia huru.
hivyo kwa uono wangu wasichana wengi wanakuwa waoga wa kukataa kwa sababu wanaamini kuwa wakimkosa leo kesho atakuwa keshachukuliwa na mwingine. Siku hizi hakuna cha "NAMWOGOPA BABA" au "TWENDE KWANZA KWA WAZAZI", kwanza wanaume wa siku hizi pia hawapendi longo longo.