Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,851
- 9,472
Nitangazie shida zako basi nikutoe
aka! Sahv sina shida.lol!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nitangazie shida zako basi nikutoe
hapo imeeleweka sasa, ile dizaini mama mgonjwa nahitajika cjui shs ngapi za hosp, cjui nn na nn hapo mna wiki mbili tu za mahusiano lakini umesushiwa matatizo debe, inabidi tu mtu ujiulize kama ckutokea ngemweleza nani haya matatizo au angeyatatua vipi?
Rafiki uliingizwa mjini pole sana halafu wewe ni wa bara eee! huwa mnahonga tu haijalishi niniSikia story hii ya ukweli:
Kaka yangu (mtoto wa mama mkubwa) alikuja Dar miaka kadhaa iliyopita kufuatilia malipo ya marekebisho ya mishahara baada ya kupandishwa cheo. Akakutana na mdada mmoja akiiishi au akija jirani na kwetu (sina uhakika ila nilikuwa namfahamu kwa sura). Brother akadondokea hapo. Siku ya kwanza kabisa, mdada akadodosa akajua sababu ya "wakuja" huyu kuwepo Dar - btw Kiswahili cha kwetu kinajulikana tu - na akaanza ukaribu wa ajabu. Brother akawa ananyweshwa bia na kula nyama, akitaka kulipa bibie anasema "acha tu nitalipa, wewe ni mgeni wetu. Kwani nikija huko kwenu nitalazimika kujilipia takrima?"
Siku brother alipopata pesa yake, akamnunulia mwali kijizawadi, lakini alipofika mahali mdada alipokuwa anapaita ni kwake akamkuta analia: "Sijui nikwamie vipi, mama yangu anaumwa sana Morogoro. Hivi wananisubiri mimi tu na sijui kama nitamkuta yu hai". Brother akatoa laki - naongelea laki ya 1995. Jioni ya siku ileile tupo mitaa ya Msisiri, tunamuona mtu mwenye mama mgonjwa! Hakuonekana tena mitaa ya kwetu kwa siku kadhaa.
The moral of story: Ukianza kuliliwa shida wewe jua kinachoendelea. Huhitaji kuchorewa picha - hata kama hujui kusoma/kuandika.
Rafiki uliingizwa mjini pole sana halafu wewe ni wa bara eee! huwa mnahonga tu haijalishi nini