Naomba kama mtu aliyeoa ila mwenye maadili ni COMMENT. Mwanaume aliyemwaminifu anapooa akili yake inamwambia kwamba mkeo atakupa kila haki ya kimapenzi uliyokuwa unaikosa ukiwa single. Pia mkeo atakuwa mshauri mkuu wa masuala yote yatakayohusu mustakabali wa maisha yenu yote including watoto kama Mtajaliwa Na Mungu.
Pia katika ndoa ni furaha , maelewano na amani huku zikiwepo changamoto ndogondogo.
Uzoefu unaonyesha baada ya wanandoa kukaa kwa takribani 5 years huwa wanazoeana na mara nyingi akina mama huwachoka waume zao haraka sana na kuanza kufanya mambo "business as usual" huku men wakijitahidi ku-maintain ile ahadi ya ndoa yao.
Akina mama wanapoanza kufanya mambo ki- business as usual wanaume wengi huumia na hapa migogoro ya kwenye ndoa huanza huku akina mama wakiwa wabishi kuliko kitu chochote. Ubishi wa akina mama unawasababisha kushindwa kufanya hata review ya tabia zao na kuamua kushikilia misimamo yao kwa kutotaka kuambiwa wala kubadilika kwa lolote.
Hali hii huwakatisha tamaa wanaume wengi na hapo jicho lao lina shift kutoka kwa mkewe kwenda kwa wanawake wengine kwa sababu wanahisi usaliti ndani ya nyumba. Kuanzia hapa wanaume hujikuta wakianza mahusiano nje ya ndoa tena mengi kuliko kabla hawajaoa. Kwa hiyo tatizo la kutoka nje ya ndoa kwa wanaume lina sababishwa kwa kiasi kikubwa na tabia za wanawake wao.