Wanawake wanasaidia wanawake?

Wanawake wanasaidia wanawake?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kabla Tanzania hatujaamua kuwa na 50-50% ya kila jambo kati ya wanaume na wanawake hetu tutizame nyuma kwanza tuone kile kiwango tulichokwisha kiteleleza kina hali gani?

Tujadiliane ili tuone kama ni kweli wanawake wakiwa 50% kwenye taasisi zetu kutatoa unafuu kwa wanawake wengine waliowengi nchini? Hebu tuone zile taasisi ambazo tayari zinaongozwa na wanawake kama vile majimbo, wizara, shule, mahakama na makampuni kama zimetoa ahueni yoyote kwa wanawake wenzao nchini kuanzia vijijini hadi mijini zikilinganishwa ta taasisi kama hizo lakini zinazoongozwa na wanaume. Je, wanawake viongozi wanawasaidia wanawake wenzao?

Kwa muono wangu mimi sioni tofauti yoyote ila ninachoshuhudia ni maringo, vijembe na mipasho kati ya wanawake wenye madaraka na wasiokuwa nayo, pia kujilimbikizia mali, vipodozi, kwenda saloon kila mara na kuhonga na kuchukua vijana wa kiume na mabwana za watu kwa baadhi ya wanawake wenye madaraka huku hali halisi za wanawake wenzao zikibaki vile vile kwenye taasisi zinazoongozwa na wanawake wenzao.

Kinachowarudisha nyuma wanawake sio wanaume bali hali yao ya kuwa wanawake inayowalazimu watembee na vioo, shedo, lotion, wanja, khanga, vilemba, mitandio, heleni, bangili na... kwenye mikoba yao kila mahali na kila wakati, vitu hivi vinawapotezea muda wao mwingi wa kufikiri na kutenda mambo yanayowahusu wanawake wenzao, maana kila wakati wanawake hawapendi kuona yuko mwanamke anayemzidi kwa kwa lolote kuanzia mkoba, kiatu, mavazi, saloon, n.k. Hii ni tofauti na wanaume ambao tangu achane nywele zake asuhi anakutana nazo tena kesho asubuhi, mwanaume hana tabia ya kuwaza mwanaume mwenzake kavaa saa, suluari wala kofia gani, hii inampa fursa ya kuwaza na kutenda mambo yake na yawengine pia.

Hebu tuangalie nyuma tuone kama tunahitaji 50-50 au tuiachie nature to take its own coarse bwetween males and female kwa kuondoa vizingiti vinavyowanyima wanawake na wanaume fursa sawa za kupata elimu na kuajiriwa badala ya kulazimisha wanawake wawe 50%
 
Naomba mtu anipe summary plz

Anawasifu wanaume kuwa wakichana nywele leo asubuhi hawazigusi tena mpaka kesho asubuhi wakati wanawake wanaenda saloon kila baada ya dkk 5
 
Back
Top Bottom