Wanawake wanawataka wanaume wa kuishi nao na sio watu wenye jinsia ya kiume, vijana wengi hawaelewi hili

Wanawake wanawataka wanaume wa kuishi nao na sio watu wenye jinsia ya kiume, vijana wengi hawaelewi hili

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Siku hizi kundi la team kataa ndoa linazidi kukua kila kukicha lakini wengi hawajui kiini cha tatizo ni nini?

Lipo kundi la watu wachache ambao kweli ni halali kwao kususia/kukataa kuoa kutokana na madhira waliyokutana nayo au waliyoyaona kwa watu wao wa karibu.

Lakini kundi kubwa lililobaki la team kataa ndoa wengi hawautendei haki uanaume wao.

Mwanaume umeumbwa kuwa leader na sio follower lakini sasa wengi wanaofanya kinyume chake, yani utakuta mtu mpaka pesa zake alizozitafuta kwa jasho anatunziwa na mkewe na mkewe anampangia matumizi ya hizo pesa.

Utakuta mtu mwanaume lakini hata kumkaripia mwanamke anapokosea hawezi, utakuta mtu mwanaume lakini shida ndogondogo zinazotokea nyumbani hawezi kuzitatua mpaka apate msaada kwa wanaume wenzake , inafika pahala hata kubadili bulb tu hawezi mpaka aite fundi.

Utakuta mtu hawezi kujiongeza kwa chochote ili asonge mbele kimaisha,miaka nenda miaka rudi maisha yake ni yaleyale hata kupiga hatua japo kidogo hawezi.

Unakuta mtu amezubaa zubaa mkewe ana mzidi akili kwa vitu vidogo sana.

Ulimbukeni na kupenda kusifia sifia hovyo wanaume wenzake wenye maisha mazuri.

Kumpenda mwanamke kuliko anavyojipenda yeye, mambo yake hatimizi anatimiza ya mkewe tu.

Kuwa legelege, mwanaume aliyelegea legea ni ngumu sana kupendwa kwa dhati na mwanamke, maana sifia kubwa ya mwanaume ni ulinzi na muonekano strong,kweli hapo hata akikuangalia ataona kabisa nipo na kidume.

Acha kumkubalia kubalia hovyo kila jambo unaloambiwa na mke wako,maana halisi ya leader hapo inaondoka utabaki kuwa follower tu na lazima akutapeli akatafute kidume kingine kiwe leader wake maana mwanamke ameumbwa kuongozwa na si kuongoza.
 
Brother mbona wapo wanaume wengi wanahizo sifa unazosema ila bado wanateswa na wake zao.

Hayana formula ukiingia kwenye engo zao lazima ukatae ndoa
 
Unakuta mtu amezubaa zubaa mkewe ana mzidi akili kwa vitu vidogo sana
Madogo siku hizi wanaanza mapenzi hata Condom haziwatoshi, Yaani Condom zinapwaya.

Mwanamke anao uwezo wa kujua udhaifu wa mwanaume mapema sana, na wanawake wamejua udhaifu wao, so wanawanyoosha vijana kisawasawa hadi akili ziwakae sawa.

Naungana Mkono na Wanawake katika kuwanyoosha vijana wa hovyo, Maana Mtu ispomfaa akili yake utamdhuru Ujinga wake. Tukishauri humu wanatuona sisi kama wakata viuno wa akudo, wanapuuza.

WOMEN, Keep it up. Endeleeni kuwanyoosha vilivyo hadi yowe lisikike. Kichwa kisicho na akili ni adhabu kwa miguu.
 
Mbona wanaume wa Zanzibar wemeregea regea lakini wanadumu kwenye ndoa
 
Back
Top Bottom